habari Mpya


Lori la Mizigo la pinduka katika daraja la Kyaka barabara ya kuelekea wilayani Karagwe mkoani Kagera.

MISENYI:Na Shaaban Ndyamukama
Kama waswahili wasemavyo kufa kufaana ndivyo ilivyojitokeza kwa wakazi wa mji wa Kyaka wilaya ya misenyi Mkoani kagera waliponufaika na ajali ya gari lililoponduka katika daraja la Kyaka barabara ya kuelekea wilayani Karagwe.

Wakazi hao wamesomba kreti za bia baada ya Lori lenye namba za usajili T.464 BWZ kupinduka katika daraja hilo likitokea Dar es Salaam kwenda Karagwe majira ya saa 10 jioni  ambapo dreva na utingo walinusurika kifo japo walipata majeraha madogo
Aidha gari hilo lilikuwa na tela lake lenye namba za usajili T.898 DDLambalo pia lilijaa kreti za bia vyote kwa pamoja vilipinduka kutokana na uzito wa mzigo ambapo kiwango cha tani hakikutajwa

Inaelezwa baada ya ajali kutokea watu walibeba chupa za bia na kukimbia nazo majumbani hadi jeshi la polisi lilipofika na jeshi la akiba (mgambo) kuimarisha ulinzi na usalama ambapo baadhi ya kreti za bia zilimwagika kwenye daraja 

Dreva wa Lori hilo Samwel Gendo licha ya kukataa kuhojiwa na waandishi wa habari alikiri kupoteza mwelekeo wakikata kona katika daraja na kushindwa hatimaye gari kuanguka.

"Watu walibeba bia na kukimbia nazo hadi askari walipofika hali ikatulia lakini baadhi wamelewa vya bwelele" Alisema mmoja wa waliokuwa katika ajali hiyo

Askari wa jeshi la polisi wamekutwa eneo la tukio wakilinda usalama wa Mali hiyo na dreva wakiwasiliana na mmiliki wa hilo gari kuweza kupata sulihisho la safari iliyoishia katika daraja la barabara ya Kyaka kwenda Karagwe.Post a Comment

0 Comments