habari Mpya


Lori la gonga Dala dala 3 nakusababisha Watu 20 kufariki na Majeruhi 45 mkoani Mbeya

Mbeya:na mwandishi wetu.
  
Watu 20 wamefariki papo hapo na 45 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea Mlima Iwambi/Mbalizi-Mbeya ikihusisha magari manne zikiwamo daladala 3 na lori moja.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amesema  ajali iliyotokea leo mchana eneo la Mteremko wa Mlima Mbalizi-Mbeya ambapo Lori hilo liligonga daladala tatu zilizokuwa zikitoka standing ya mbalizi kuelekea mbeya mjini 

Amesema ajali hiyo imesababisha  vifo hivyo na majeruhi hao ambapo gari la contena liligonga daladala tatu za abiria na kwamba wananchi na askari wa vikosi vya ulinzi na usalama wamehusika kusaidia kuopoa miili ya marehemu na majeruhi kukimbizwa hospitali.


Pia mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiongozana na vikosi vya JKT & JWTZ wako eneo la tukio wakifanya mawasiliano ya kupata vyombo vya usafiri kuwahisha madaktari hospitali ya mkoa kutoa huduma na kuhamasisha wananchi kufika kitambua miili ya ndugu zao lakini kutoa msaada wa damu kwa waliojeruhiwa.

Wakati huohuo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakt.John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la mawaziri Ambapo sasa:.
Kangi Lugola – Aekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi 
Musa Ramadhani Sima - Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais 
Omary Mgumba - Naibu Waziri wa Kilimo 
Prof.  Makame Mbarawa - Waziri wa Maji na Umwagiliaji 
Mhandisi Isack Kamwelwe - Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano 
Athumani Kihami - Katibu wa Uchaguzi NEC


Post a Comment

0 Comments