habari Mpya


Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera imeshauriwa kuhamasisha wakazi wa wilaya hiyo kuzalisha wa matunda aina ya parachichi

NGARA: Na Shaaban Ndyamukama Rk.
 Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera imeshauriwa kuhamasisha wakazi wa wilaya hiyo kuzalisha wa matunda aina ya parachichi ili kuweza kujiongezea mapato kiuchumi badala ya kutegemea zao hilo kutoka nchini Burundi.

 Mmoja wa wafanya biashara wa mji wa kabanga wilayani humo  Said Abdallah ametoa ushauri huo wakati akiongea na waandishi wa habari na kwamba biashara ya maparachichi imeshamiri kwa  kuwainua wananchi kiuchumi ngazi ya familia.

Abdalla amesema vijana waliojiunga kwenye Vikundi na kuanzisha ujasiliamali wa kuuza parachichi   kwa siku  wanasafirisha magari 10  ya zao hilo kutoka nchini Burundi  ambapo  halmashauri hupata ushuru Sh450 000 kwa  gari moja.

Amesema kwa kila gunia halmashauri   hukusanya ushuru wa Sh1,500 kwa kila gunia na matunda hayo husafirishwa  mikoa ya  Shinyanga, Singida, Dodoma na Dar es salaam na halmashauri huingiza mapato ya Sh4.5 milioni kwa magari 10.

Said Abdallah amesema mji wa kabanga unamiliki maduka 200 ya wafanya biashara lakini kati ya hayo maduka 50 yamefungwa kwa kukosa wateja huku wakitakiwa kulipia ushuru wa halmashauri na wateja wao wanatokea Burundi .

“Serikali iweke mkakati wa kibiashara wa kuruhusu raia wa Burundi kufuata utaratibu rahisi wa kuingia na kuanzisha biashara ya kuuza bidhaa na kuingiza ushindani kimapato kwa nchi zote wakilipa kodi stahili”Alisema Abdallah

Pichani ni mmoja wa wafanya biashara Said Manywele kuto mji wa kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera. 
 Mwenyekiti wa wafanya biashara wa mji huo  Samwel George amesema  wafanyabiashara hao wanauziana bidhaa  na wezao kutoka  Burundi lakini  nchi hiyo imeongeza ushuru na kodi kwa bidhaa zinazotoka Tanzania.

Amesema hali hiyo imesababisha washindwe kuhimili viwango hivyo mji wa Kabanga umeshuka kimapato nakushauri  mamlaka zinazohusika nchini Burundi kupunguza ushuru au kodi kwa  mchele na mafuta ya kupikia kunufaisha wafanyabiashara wa pande mbili zilizo jirani.
Pichani ni Mwenyekiti wa wafanya biashara wa mjiKabanga Samwel George. 
Alisema  changamoto  nyingine ni vizuizi vinavyowekwa na halmashauri inayowatoza ushuru wajasiriamali wadogo kutoka nchi jirani kwa kuwatoza fedha kubwa wakikusanya mapato ya ndani na kufikia hatua ya kufilisika mitaji yao.

“Hatujafaidika kibiashara ndani ya jumuia ya Afrika Mashariki kwa sababu warundi wanalazimika kusafiri mpaka mikoa ya ndani ya Tanzania kununua bidhaa zinazopatikana hapa Kabanga na sisi kukosa wateja” Alisema George
Inadaiwa  wajasiriamali wadogo wanatozwa fedha na mamlaka ya mapato (TRA) pamoja na ushuru wa halmashauri ambapo kila kibanda cha biashara hulipia Sh10,000 kila mwezi  bila kuangalia mapato ya mfanyabiashara husika. 

Pia wafanyabiashara wa mji wa kabanga wameishauri halmashauri ya wilaya kuingia ubia na wadau wa kibiashara kukamilisha soko la kimataifa lililotelekezwa katika mpaka wa Tanzania na Burundi uliolenga kunufaisha Afrika Mashariki.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Aidan Bahama alisema soko la kimataifa ambalo ni  soko la kimkakati lilijengwa na serikali kuu na kutokea changamoto ya uhaba wa fedha hivyo kunahitajika wawekezaji wakulimalizia.


Alisema wakijitokeza wafanya biashara wanaoweza kuungana pamoja na kuwekeza fedha zao kulikamilisha na wao watapata hisa katika uendeshaji wake kwa kuunganisha nguvu za halmashauri na wadau wengine wanaoweza kujitokeza. 

“Wilaya hii inao wajasiriamali na wafanyabiashara 1,600 wenye  maduka ya rejareja na bidhaa za jumla hivyo wakipatikana  wenye fedha  hatimaye kukafanyika kongamano la kibiashara Afrika Mashariki watanufaika” Alisema
Hata hivyo wananchi na wafanya biashara walipongeza mahusiano yaliyopo baina ya wafanyabiashara wa wilaya ya Ngara na nchi jirani ya Burundi katika suala la ulinzi na usalama na kwamba hali hiyo inawafanya kuwa pamoja kiuchumi.Post a Comment

0 Comments