habari Mpya


MKURUGENZI Biharamulo:Soko la mmalaka ya mji mdogo wa biharamulo nichafu,usafi ufanyike haraka iwezekanavyo.

Na Shaaban Ndyamukama Rk Biharamulo.
Vongozi wa mamlaka ya mji mdogo wa biharamulo mkoani Kagera wameshauriwa kifanya usafi wa mazingira mara mbili kwa wingi kutokana na msonhamano wa wananchi wanaojihusisha na masuala mbalimbali ya kijamii.

 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Wende Ng'ahala amesema uchafu mwingi unapatikana kwenye soko la mamlaka ya mji ambako ndipo kioo cha mji na wilaya hiyo
Ng'ahala amesema pia wajitahii kichimba mashimo ya kutunzia takataka zinazo weza kutumika kama mbolea ya kupandia mazao wakati wa msimu wa kilimo lakini kuhifadhi mandhari ya mazingira
Amesema watendaji idara ya usafi na mazingira ya mamlaka hiyo wamepewa mamlaka ya kutumia sheria za halmashauri hiyo na zilizobainishwa na serikali kuu kuwachukulia hatua wanaokaidi kutunza mazingira katika maeneo yao
"Sehemu ya lile soko linajumuisha wakulima wanaouza mazao na wachuuzi wa matunda lakini wanunuzi na wafanyabiashara hawashirikia kuweka uchafu kwenye vizimba" Amesema Ng'ahala
Kizimba cha soko kuu la biharamulo limezidi kuwa kero kwa kujaa uchafu au takataka na kusababisha ndehe pori kufurika kutafuta mizoga na uchafu kama mabaki ya vyakula vinavyotupwa na wenye mighahawa au wauzaji wengineo

Pia soko hilo limekuwa kimbilio la mifugo hasa mbuzi hata kama wajasiriamali wakijitolea kufanya usafi na kuwalipa vibarua kusomba takataka kuelekea maeneo yaliyotengwa kuzihifadhi kuepukana na harufu mbaya 

Post a Comment

0 Comments