habari Mpya


Balozi wa uholanzi nchini Tanzania Jeroem Verheul Afanya ziara wilayani Biharamulo mkoani Kagera.

BIHARAMULO: NA SHAABAN NDYAMUKAMA  RK.

Serikali imeridhia majaribio ya ujenzi wa Barabara inayojengwa kwa kiwango cha udongo kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika halmashauri ya wilaya ya biharamulo mkoani kagera chini ya ufadhili wa ubalozi kutoka nchini uholanzi iliyoanza kujengwa February mwaka huu.

Naibu waziri wa Tamisemi   Joseph Kandege amesema teknolojia iliyotumika kujenga barabara ya Rukaragata katika mamlaka ya mji wa Biharamulo  yenye umbali wa kilomita moja kwa thamani ya shilingi milioni 39 za kitanzania itakuwa na uwezo wa kukaa na kutumika kwa kipindi cha   miaka 5 mpaka minane bila kuharibika

Kandege akiongea na baadhi ya viongozi wa chama na serikali hii leo wilayani Biharamulo amesema majaribio ya ujenzi wa barabara hiyo ni ya mwanzo kwa nchi ya Tanzania na kwamba kama utafiti unavyoonyesha huenda kilomota zikaongezwa kutengeneza kwa umbalo zaidi ili kuokoa fedha za kutumika kila mwaka ndani ya halmashauri hiyo
Imeelezwa kuwa ukarabati wa barabara kwa halmashauri hiyo kwa kiwango cha changarawe kilomita moja hutumia thamani ya Shilingi milioni 15 hadi 18 kwa muda wa miaka mitatu na kwamba kutakuwa na unafuu wa kiuchumi katika kutumika kwa barabara zenye teknolojia ya kisasa ambazo zitasaidia kuhudumia wananchi kwa haraka.
"Mara nyingi serikali ikipata wawekezaji kama hawa hatuna budi kutunza miundombinu inayojengwa na kuweka mipango ya kukuza uchumi kama kuanzisha viwanda kwenye maeneo ya wananchi ili mazao yanayolimwa yatumike kuzalisha bidhaa zaidi" Alisema Kandege

Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita tano inatarajia kuhudumia vitongoji vya Rukaragata na Rubondo vyenye wakazi 4000 wanaohitaji huduma za masoko ya mazao na huduma nyingine za kijamii  ndani na nje ya mamlaka ya mji wa Biharamulo.

Balozi wa uholanzi nchini Tanzania Jeroem Verheul amesema viwango vilivyotumika kiteknolojia  kujenga barabara ni  kuparua kwa upana na kuishindilia udondo wa mfinyanzi unaochanganywa na kemikali kisha kushindiliwa ikikaa miezi sita  kwa matazamio ikiendelea kutumika.

Amesema teknolojia inayotumika  manufaa yake yataanza kuonekana kuanzia miaka sita hadi 20 kwa uimara wa barabara na kwamba itarithishwa kwa  wakandarasi na wahandisi wanaofanya kazi na Tarura kote nchini Tanzania.

Mbunge wa jimbo la Biharamulo Mkoani Kagera Oscar Mukasa amesema nchi ya uholanzi iliamua kujenga barabara kwa halmashauri hiyo baada ya kupokea maombi yake kwa lengo la kusaidia jamii kupata huduma za kijamii na kupunguza umaskini

Mukasa alisema wilaya hiyo ni ya pili nchini Tanzania kwa imaskini unaotokana na kukosa miundombinu ya kuwafikia wakulima wenye mazao mengi yanayokosa soko kwa sababu ya barabara na mazao hayo kuharibika kwenye makazi yao


"Kazi ya mbunge ni kutafuta fursa za kusaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na kupata  huduma bora za kjamii kama elimu, afya na maji kwa kupita  njia zenye usalama na rafiki kiutendaji. Alisema Mukasa

Pia katibu mwenezi wa chama cha Mapindizi mkoa wa Kagera Hamimu Mahmoud na alisema kama mpango huo ni vema ukaelekezwa mazingira ya wananchi walioko vijijini kusaidia akina mama na watoto wanaokwenda kutafuta huduma za afya mbali na makazi yao.


Alisema serikali itatumia fursa hiyo kuhamasisha Sera ya uchumi wa viwanda kwa kuwepo barabara imara zinazowafikia wananchi na kuwavutia wawekezaji kuharakisha maendeleo ya wilaya ya Biharamulo kupunguza umaskini.

Post a Comment

0 Comments