habari Mpya


Waziri Mkuu asema Vipaji vya Michezo na Sanaa Vitaitangaza Nchi Kimataifa na Kuongeza Fursa ya Ajira kwa Watanzania.

Mkurugenzi Nyanza Bottling Company Ltd  Christopher Gachuma akisalimaina na Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Na Kosta Kasisi –Radio Kwizera 97.7 Mwanza.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Jana (Jumamosi, Juni 9, 2018)  amefungua rasmi Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania  (UMISETA) yanayofanyika kwenye  Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Waziri Mkuu amewataka Viongozi wa Mikoa na Wilaya zote nchini wahakikishe kuwa masomo ya haiba, michezo na stadi za kazi yanafundishwa kikamilifu kwenye shule zote za msingi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema somo la elimu ya michezo kwa Shule za Sekondari nalo lifundishwe kikamilifu na vyuo vya michezo kama Malya viendelee kuwaendeleza walimu wa michezo.
 
Kaulimbiu ya Mwaka huu 2018 inasema MICHEZO ,SANAA NA TAALUMA NI MSINGI WA MAENDELEO YA TAIFA .

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amewaagiza Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya wahakikishe maeneo ya michezo na burudani yanapimwa na yasiingiliwe, pia vitengo vya michezo kwenye ofisi za Halmashauri na Mikoa vitengewe fedha za kuendeshea michezo.
 
 
 
Wanafunzi wa UMISETA  wakiimba wimbo wa alaiki uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Waziri Mkuu amesema vipaji vya michezo na sanaa vitaitangaza nchi kimataifa na kuongeza fursa ya ajira kwa Watanzania. Amesema kauli mbiu ya michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA ya mwaka  huu ni “michezo, sanaa na taaluma ni msingi wa maendeleo ya mwanafunzi  katika Taifa letu”.
 

Post a Comment

0 Comments