habari Mpya


Watu 5 wafariki papo hapo na wengine 36 kujeruhiwa baada ya Basi la Abiria kuacha njia na kupinduka mkoani Geita

Na mwandishi wetu Gibson Mika
Watu wa 5 wamefariki na wengine 36 kujeruhiwa  baada Gari la abiria (BASI) aina ya YUTONG  kuacha njia na  kugonga  Gari dogo aina ya Toyota Haria lililokuwa likitokea Mjini Geita kuelekea Jijini Mwanza   katika eneo la Kata ya  Buharahara Wilaya ya Geita mkoa wa Geita.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani humo Mponjori Mwabulambo amesema kuwa tukio hilo limetokea Juni 17, 2018 majira ya saa nne asubuhi katika kata hiyo na kuhusisha gari la kubeba abiria BASI lenye namba za usajili T 204 CGW aina ya YUTONG mali ya king Msukuma lililokuwa ikitokea Mkoani Mwanza kuelekea Mkoani Kagera na  gari dogo aina ya Toyota  haria yenye namba za usajiri T907 DLG iliyokuwa ikitokea  Mjini Geita kuelekea Jijini Mwanza.
 Pichani ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita Mponjori Mwabulambo
 Nikweli mnamo juni 17,2018 majira ya saa nne asubuhi huko katika eneo la Buharahara hapa wilayani Geita kumetokea ajali iliyolihusisha basi lenye namba za usajili T204 CGW aina ya Yutong mali ya Msukuma lililokuwa likitoka Jijini Mwanza kuelekea mkoani Kagera limeligonga gari dogo aina ya Haria lenye namba za usajili T907 DLG lilokuwa likitokea Geita kwenda jijini Mwanza”amesema Kamanda mwabulambo.
Basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Dereva aliyejulikana kwa jina la Mwita Chacha huku dereva wa gari dogo aina ya Toyota haria lilikuwa linaendeshwa  na  Maiko Kabaya na kwamba baada ya kufika katika eneo hilo dereva wa basi alihama njia na kwenda upande wa pili kisha kugoga gari hilo dogo lililokuwa likitokea Mjini Geita kuelekea  Jijini mwanza.


 Pichani ni Basi lililo pata ajali
Abiria waliokuwa ndani ya basi hilo walikuwa ni 58 kati yao watano wamepoteza maisha papo hapo na wengine 36 wamejeruhiwa na kwamba kati ya majeruhi hao majeruhi  watano wamepewa rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali ya Bugando liliyopo mkoani Mwanza baada ya hali zao kuendelea kuwa mbaya.
Kati ya majeruhi hao,  waliopewa rufaa wanaume ni 4 na mwanamke mmoja. Na waliopoteza maisha  wote ni  wanawake, akiwemo mtoto mdogo mwenye umri wa miezi sita na mwanamke mmoja ambaye alikuwa akitembea kwa mguu kutokea mjini Geita.Watu waliokuwa kwenye gari dogo wametoka wakiwa salama na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa geita baada ya kile kilichoelezwa kuwa walikuwa wamefunga mikanda iliyopo kwenye viti vyao.
Ajari  hiyo inatajwa na kamanda huyo kuwa ajari kubwa na mbaya ndani ya kipindi cha muda wa miaka mitatu kutokana na vifo hiyo pamoja na idadi za majeruhi.
Baadhi ya abiria waliokuwemo kwenye basi hilo, zawadi mgaya na Agripina prospa wamesema dereva wa basi alikuwa mwendo wa kawaida na kwamba wengi wao waliopoteza maisha walikuwa hawajafunga mikanda.
Kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali teule ya Mkoa wa Geita Mazoea Kimbo amekiri kupokea miili ya watu watano, wote wajinsia ya kike na majeruhi 36 kati ya hao, wanaume 18 na wanawake 18 na kwamba  watu watano wamepewa rufaa ya kwenda kutibiwa bugando wanaume 4 na mwanamke mmoja na waliobakia hospitalini hapo hali zao  zinaendelea vizuri.
"Nikweli tumepokea miili ya watu watano walio fariki kutokana na ajali hii tumewahifadhi katika chumba cha kuhifadhia Maiti na majeruhi watano tumewapa rufaa kwaajili ya kwenda kutibiwa Hospitali ya Bugando Jijini Mwanza " Amesema Dakt.Kimbo.
 
Mkuu wa mkoa wa geita Mhandisi Robart Gabriel  ametoa wito kwa abiria kufunga mikanda wanapokuwa safarini  kutokana na wengi wao waliokuwa wamefunga mikanda iliyo kwenye viti vyao  kutoka wakiwa salama.Post a Comment

0 Comments