habari Mpya


Watakao kutoa Hati za Kusafiria za Kielektroniki Kinyume na Sheria Kuchukuliwa Hatua Kagera.

Kamishna wa Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga (Kushoto) Akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kinawilo  Pasipoti ya Kielekitroniki Baada ya Uzinduzi.


 
Maofisa wa Idara ya Uhamiaji Wakisikiliza Kwa Umakini Hotuba ya Uzinduzi wa Pasipoti za Kielekitroniki Mkoani Kagera.

Serikali ya Tanzania imesema haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria Watumishi wa Uhamiaji watakaobainika kushirikiana na viongozi na watendaji wa vijiji kutoa hati za kusafiria za kielektroniki.

Hayo yameelezwa na Kamishina wa Uhamiaji anayeshughulikia Hati na Uraia Bw Gerard Kihinga wakati wa uzinduzi wa huduma ya Paspoti ya kielektroniki Mkoani Kagera June 8,2018 uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa Manispaa ya Bukoba.

Amesema hati hiyo ni kwa ajili ya Watanzania pekee lakini wapo raia wa kigeni wangependa kutumia pasipoti hiyo kuishi nchini kinyume cha sheria ambapo amewataka watumishi kuwa waaminifu. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu, aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo amewataka Maafisa Uhamiaji kufanya kazi kwa Uaminifu na Uadilifu huku akiwataka Wananchi kujitokeza kujiandikisha ili kupata hati hiyo.

 
Picha ya Pamoja .

Unahitaji nini ili Upate Pasipoti ya Kielekitroniki?

Gharama ya Pasipoti ya Kielekitroniki ni Shilingi 150,000/=, Utajaza fomu hata ukiwa nyumbani ambayo inapatikana katika tovuti ya Idara ya Uhamiaji www.immigration.go.tz .

Viamabatanisho ni pamoja na Kitambulisho cha Taifa, Cheti cha kuzaliwa cha kwako na cha mzazi wako mmoja, Barua ya utambulisho kutoka kazini kwako/Mtendaji wa kata, Kitambulisho cha Kazi/mpiga kura, na picha tatu pasipoti size.

Post a Comment

0 Comments