habari Mpya


Wanyama Mbalimbali Pori la Akiba Kimisi na Burigi mkoani Kagera.

Baadhi ya Twiga wanaopatikana katika Pori la Akiba Kimisi mkoani Kagera.

Pori la Akiba la Kimisi lilianzishwa mwaka 2003 kwa Tangazo la Serikali namba 116 na lina ukubwa wa 1,030 km katika wilaya za Ngara na Karagwe mkoani Kagera nchini Tanzania. Pori hilo lina wanyama mbalimbali wakiwemo Tembo, Twiga, Simba na Chui.
Ndege wanaopatikana katika Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera.

Pori la Akiba Burigi lina ukubwa wa kilomita za mraba 2,941 katika wilaya za Karagwe, Muleba na Ngara mkoani Kagera.
Viboko nao wanapatikana katika pori hilo ndani ya Ziwa Burigi.

Ikumbukwe kuwa mapema mwaka huu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangala alitangaza kuanza mchakato wa kuyapandisha hadhi Mapori ya Akiba ya Burigi, Kimisi, Biharamulo, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa.

Post a Comment

0 Comments