habari Mpya


WANANCHI WAKIWA KUTOBAGUA KAZI ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI;


Pichani ni wanawake wanao jishughurisha na upondaji wa kokoto na kuuza.
NGARA : Na Shaaban Ndyamukama.
Jamii imetakiwa kutobagua kazi halali zinazoweza kuwaingizia kipato na kupunguza changamoto za familia ikiwa ni pamoja na wanawake kufanya kazi wanazoweza  kuliko kuwa na maisha tegemezi

Hayo yamebainishwa na kikundi cha wajasiliamali wanaogonga na kuuza kokoto katika kitongoji cha Goyagoya kata ya Rulenge wilaya ya Ngara mkoani Kagera ambao huuza gari moja kwa thamani ya Shilingi 40,000 na kujikwamua kiuchumi


Baadhi ya  wanawake wanaogonga kokoto katika  kitongoji hicho Agnesta Jonas  na Hadija Ismail  walisema wamejiajiri  kupata  mahitaji muhimu  ya kifamilia kama mavazi, vifaa vya shule kwa  watoto  hasa madaftari na sare za shule.

Aidha badhi ya wanaume wanaoshiriki uchimbaji wa mawe na kugonga kokoto walisema wamefanya shughuli hiyo na kuwea kupata fedha za kununua bidhaa nyingine kama maharage na mabati ya ujenzi wa nyumba bora za kuishi.

Ismail Rajabu alisema yeye alisema katika kipindi cha  miaka saba ameweza kujenga nyumba bora kupata usafiri wa pikipiki  ambapo aliwataka vijana kufanya kazi za ujasiliamali wakitumia rasilimali zinazopatikana kwenye mazingira yao.


 Pichani ni diwani wa kata ya Rulenge Hamis Baliyanga akitoka mlima kuzungumza na wananawake waponda kokoto kwaajili ya biashara.
Kwa upande wake diwani wa kata a Rulenge Hamis Baliyanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu anavyoweza kusaidia kikundi hicho cha wagonga kokoto alisema kama watakuwa kwenye umoja wao wanaweza kusajiliwa na kupata mkopo kutoka Halmashauri kupanua na  kuendeleza mradi wao


Hata hivyo alishauri pamoja na kuuza kokoto wajitahidi kutunza mazingira kwa kufukia mashimo na kutokata miti ovyo na kwamba anawapongeza wanawake ambao walijiunga pamoja  na wanaume kufanya shughuli hiyo  ya uzalishaji mali

Post a Comment

0 Comments