habari Mpya


Wananchi Ngara Shirikini kulinda Vyanzo vya Maji.

Picha Na Mohamed Makonda.

Wananchi Wilayani Ngara Mkoani Kagera wametakiwa kushirikiana na serikali kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa kwa kupanda miti na maua ili kuweka mazingira safi na salama.

Hayo yamesemwa hii June 5, 2018 na Bw Moris Mombia Afisa tarafa wa Rulenge kwa Niaba ya Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanal Michael Mtenjele katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, yaliyofanyika kiwilaya kwenye mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge. 

Bw Moris Mombia  amehimiza kuweka msukumo wa pamoja katika kuhamasisha Jamii, kuhifadha na kutunza mazingira ili kudhibiti uhalibifu mkubwa wa mazingira unaopelekea mabadiliko ya tabia nchi.

 
 
Nae Afisa Usafi na Mazingira Wilayani Ngara Bw. Waziri Nicholaus amesema elimu imetolewa kwa wadau wa mazingira waweze kuhamasisha jamii kutunza na kusafisha mazingira huku akisisitiza matumizi ya nishati mbadala kwa lengo la kupunguza matumizi makubwa ya mkaa yanayosabisha uharibifu wa mazingira

Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani hufanyika Juni 05 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu imeadhimishwa chini ya kauli mbiu inasemayo MKAA NI GHARAMA TUTUMIE NISHATI MBADALA.


Post a Comment

0 Comments