habari Mpya


Wananchi Buhigwe wapokea Hatimiliki za Kimila za Ardhi.

Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti akikagawa hatimiliki kwa Mwananchi.


 
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti akionesha hatimiliki kwa Wananchi kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

 Picha zote Rhoda Ezekiel.

Halmahsuri ya wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma imeanza zoezi la ugawaji wa hati miliki za kimila katika vijiji vya Mugera, Kajana na Katundu katika kata ya Mugera na Kajana katika kaya 1025 hati ambazo zitasaidia kupunguza migogoro ya ardhi katika wilaya na mkoa kwa ujumla.

Akikabidhi hati miliki hizo kwa kaya 50 za mfano June 3, 2018 katika kijiji cha Muhegera kata ya Mugera wilayani humo, zinazotolewa na mradi wa usimamizi wa maliasili kwa ajili ya kuongeza kipato kwa Mwananchi unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania na Ubelgiji chini ya shirika la ENABEL, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kigoma, Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti alisema katika kesi 10 zinazofika ofisini kwake kati ya hizo 8 ni za migogoro ya ardhi na mbili ni za urithi.

Brigedia Jenerali Gaguti alisema mradi huo utasaidia usalama wa wananchi na kupunguza migogoro ya ardhi ambayo ilisababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na wengine kubaki wakiwa walemavu kwa kugombania ardhi.

 
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti akikagawa hatimiliki kwa Mwananchi.

 
 Brigedia Jenerali Marco Gaguti  amewataka Viongozi wa vijiji kusimamia ipasavyo maeneo ya huduma za kijamii yaliyopimwa kwa ajili ya shughuli za ufugaji na kilimo yatumike kwa lengo lililokusudia na wananchi waelekezwe namna bora ya kuyatumia na kuepusha migogoro kwa wananchi.
 
Akitoa taarifa ya mradi mratibu wa mradi huo wilaya ya Buhigwe, William Marandu alisema mpango wa matumizo bora ya ardhi ni tokeo tarajiwa namba mbili la mradi ilipima ukubwa wa ardhi ya Kijiji cha Mugera hekta 9401.856 chenye vitongoji vinne ambavyo ni Ruyange, Mugera, Kishaha na majengo na mradi huo ulianza mwaka 2016 kwa kutenga matumizi ya ardhi ya Maeneo ya kilimo kekari (6117.076) malisho ya mifugo Hekati 1207.1, vyanzo vya maji , maeneo ya maziko , maeneo ya makazi hekari 477.78, misitu ya asili 378 na misitu ya kupandwa hekari 1097.3 kwa kuwa Aridhi ndio chanzo kikubwa cha mtaji wa wananchi.

Alisema hati miliki zilizo gawiwa kwa kaya 50 za mfano ni kati ya hati miliki 1025 zilizoandaliwa na mradi wa (NRMLED) kwa vijiji vitatu vya wilaya ya Buhigwe na hati miliki 975 zilizobaki zitaendelea kutolewa baada ya ufunguzi wa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi wengine ambao bado hawajafanya utaratibu wa kupata hati miliki za kimila kufanya utaratibu waweze kupata hati hizo kwa kupitia Idara ya ardhi ya halmashauri ya wilaya hiyo.

 
Kwa Mujibu wa Sera ya Taifa ya Ardhi na Sheria za Ardhi Namba nne ya mwaka 1999, sheria ya ardhi ya vijiji Namba tano ya mwaka 1999 , sheria ya mpango ya matumizi bora ya Ardhi Namba sita ya mwaka 2007 kila Kijiji hakina budi kuandaa mpango wa amatumizi bora ya ardhi kwa madhumuni ya kuwezesha usimamizi na matumizi endelevu ya ardhi na maliasili na rasilimali zake zote.

Post a Comment

0 Comments