habari Mpya


Wanafunzi 231 wapata Mimba Kagera miaka 5 iliyopita.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho Meja Jenerali mstaafu Salim Kijuu.

Na-Shafiru Yusuf –Radio Kwizera Muleba.

Jumla ya wanafunzi 231wa shule za msingi na sekondari Mkoani Kagera wameripotiwa kuwa na ujauzito shuleni kwa mwaka 2014 hadi sasa.

Afisa  Elimu mkoani humo  Bw Aloyce Kamamba amesema hayo  kwenye kikao cha tathmini  ya nusu mwaka cha wadau wa  Elimu Mkoa wa Kagera ambacho kimefanyika June 1, 2018  wilayani Muleba ambapo  amesema kuwa  wanafunzi 41 ni  wa Msingi  na 190  wa Sekondari.


Afisa  Elimu mkoani Kagera, Bw Aloyce Kamamba.

 Nao baadhi ya  wajumbe ambao  ni wadau wa elimu  wameomba vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanawabaini watu  wanaowapatia ujauzito wanafunzi hao  ili  kuweza kudhibiti vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho Meja Jenerali mstaafu Salim Kijuu ameagiza halmashauri zote zifanye vikao vya wadau wa elimu kufikia July mwaka huu ili kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu mashuleni.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera,Augustine Ollomi akichangia katika kikao hicho,amewataka Wazazi,Walimu na Wadau wa Elimu mkoani humo  kushirikiana na Jeshi hilo kutoa elimu ya afya kwa Wanafunzi.

Post a Comment

0 Comments