habari


WALIMU FC YA TWAA MBUZI MNYAMA KATIKA FAINALI MAZINGIRA CUP BAADA YA KUIADHIBU BREZA FC 3-1

MULEBA NA SHAFIRU YUSUPH
Ligi  ya Mazingira cup ya kuwania Mbuzi Mnyama imefikia tamati leo kwa timu Walimu fc kujinyakulia mbuzi mnyama baada ya kufunga mabao 3-1 kwa mikwaju ya penalt dhidi ya timu ya Breza fc katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Fatuma uliopo Muleba Mjini Mkoani Kagera.

Akitoa zawadi kwa washidi hao  Mwenyekiti wa kamati ya ligi hiyo Bw.Sixbiti Samson Rubona Amesema kuwa msindi wa kwanza amejinyakulia mbuzi Mnyama mshindi wa pili shilingi elfu ishirini na mshiindi wa tatu amejinyakulia shilingi elfu kumi.

Amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa ligi hiyo ni kuhamasisha wananchi kutunza mazingira na kuchukua mshindi wa kwanza na wa pili kila tarafa ili kushiriki ligi ya wilaya ya kuwania Ng;ombe September mwaka huu ambapo wameanzia tarafa ya muleba na wataendeleo na tarafa nyingine.

Naye kocha wa timu ya walimu fc Bw.Prosco mgogoro ambao ndio washidi wa ligi hiyo ameshukuru mashabiki pamoja na wadau wa mpira wa miguu kwa ushirikiano walioutoa dhidi yao mpaka kuchukua mbuzi huyo hivyo ameomba kuendelea na ushirikiano huo.

 Kwa upande wake kocha wa timu ya Breza fc kositantine mziba amesema sababu iliyopelekea wakashindwa mchezo wa leo nikutokana mazoezi hafifu dhidi ya wachezaji na uhaba wa vifaa vya michezo ikiwemo mpira sare na vifaa vingine hali inayopeleke kutofanya vizuri kwenye michezo mbalimbali inayoendelea kwenye tarafa ya Muleba hivyo wameomba wadau mbalimbali  kuasaidia ili kuendeleza vipaji vya michezo kwenye timu hiyo.

Post a Comment

0 Comments