habari


WAKIMBIZI NYARUGUSU WAOMBA KUSAIDIWA NISHATI YA KUNI KWAAJILI YA KUPIKIA

KASULU NA KUGABI MHUBIRI.
Wafanyakazi wa mashirika mbalimbali yanayohudumia wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu wilayani kasulu mkoani wamejitokeza nakuungana na wakimbizi kuadhimisha siku ya mkimbizi duniani ambayo huadhimishwa june20 kila mwaka. 


Katika maazimisho hayo ambayo yamefanyika kwenye uwanja wa B2 kambini Nyarugusu wilayani Kasulu, Mwenyekiti wa kambi ya hiyo Bi. Abilola Tabu Angelike amepewa nafasi ya kusoma risala nahivyo kutaja changamoto mbalimbali wanazokabiliana wakimbizi Jambo ambalo ameyataka mashirika ya sheria kwakushirikiana na serikali kutafuta mbinu za kuwatatua changamoto zinazo wakabili
Ametaja baadhi ya changamoto kuwa, nipamoja na, ukosefu wa nishati yakuni kwaajili ya kupikia chakula, upungufu wa Shuleni na Walimu kulingana na ongezeko la wakimbizi na waomba hifadhi, uboreshwaji wa huduma za afya pamoja na kutatua changamoto ya upatikanaji wavyeti kwa Wanafunzi wanaomakiza kidato cha sita hasa kwa Wanafunzi kutoka nchini DRC. 

Akijibu hoja ya mwenyekiti huyo,iliyotolewa kwenye risala, mkuu wa makazi msaidizi katika kambi ya Nyarugusu,Bw. Francis Chokola ameeleza kuwa, kulingana na idadi kubwa ya wakimbizi kambini humo,serikali na mashirika wanaendelea nakujitahidi ili kuona namna ya kutatua changamoto zilizopo. 

Hata hivyo, Bw.Chokola amewataka wakimbizi waishio kambini Nyarugusu, kuendelea kuzingatia sheria za hapa nchini Tanzania ambapo pamoja na hayo ameahidi serikali kuendelea kuwalinda hadi pale amani itakapo patikana katika nchi zao za asili ili waweze kurejea kwahiari. 
Post a Comment

0 Comments