habari Mpya


Waislamu Ngara Waaswa Kuendeleza Mema ya Mfungo wa Ramadhani wakati Wote.

 
Akitoa salamu zake za Eid El Fitri leo katika viwanja vya Kokoto mjini Ngara,Sheikh Mkuu wa wilaya Ngara mkoani Kagera,Sheikh Rajabu Msabaha amesema Siku ya Idd ni siku ya kuwaangalia kwa jicho la huruma Mayatima,Wagonjwa waliomo majumbani na hata hospitalini, Wafungwa Magerezani kwa kuwatembelea na kuwasaidia kwa kila hali sambamba na kuwaombea dua ya kuwatakia afya njema, nusura ili wamshukuru Mwenyezi Mungu na wajione ni Sehemu muhimu katika sherehe hii.

 
Sheikh Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera  Rajab Msabaha akiwa na ustadhi Amir Mtenda wa Msikiti wa Istqama mjini Ngara wakiwa katila kipindi cha asubuhi njema Radio Kwizera pamoja leo June 15, 2018 katika sikukuu ya Eid el Fitri.

 
 Sheikh Rajabu Msabaha pia amewakumbusha Wailamu wote kutenda yale yaliyo yote mema yaliyokuwepo waskati wa mfungo wa ramadhani  ili kuendelea kupata Neema zake Mwenyezi Mungu.

 

Post a Comment

0 Comments