habari Mpya


Vyombo vya Habari Shirikianeni na Serikali Kuhamasisha Jamii Kuhifadha na Kutunza Mazingira Kagera.

 
Na James Jovin -Radio Kwizera Biharamulo.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Bw. Salumu Kijuu ameviagiza Vyombo vya Habari, Taasisi zote za Serikali na Asasi za Kiraia mkoani humo kuweka msukumo wa pamoja katika kuhamasisha, kuhifadha na kutunza mazingira ili kudhibiti uhalibifu mkubwa wa mazingira unaopelekea mabadiliko ya tabia nchi. 

 Hayo yamebainishwa na Kaimu mkuu wa wilaya ya Biharamulo Bw. Michael Mtenjele ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ngara akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Kagera katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani leo June 5, 2018 yaliyofanyika kimkoa katika wilaya ya Biharamulo.

 
 
Aidha katika maadhimisho hayo ya siku ya mazingira duniani Bw. Mutenjele ametoa maagizo kwa taasisi za serikali asasi za kiraia pamoja na vyombo vya habari kuhakikisha vinashiriki kikamilifu katika kutunza mazingira na kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa watu wengine.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mazingira wilayani Biharamulo Bw Michael Mkuti akisoma risara mbele ya mgeni rasimi ametaja mikakati inayofanywa na wilaya ili kuhifadhi misitu pamoja na mazingira kwa ujumla kuwa ni pamoja na upandaji wa miti ambapo kila mwaka hupandwa miti zaidi ya milioni moja katika wilaya ya Biharamulo.

Post a Comment

0 Comments