habari


Viongozi wa Dini ya Kiislamu Muleba watakiwa kutambua Nafasi zao katika Maendeleo ya Dini.

Na Shafiru Yusuf – RK Muleba.

Viongozi wa dini ya kislamu Wilayani Muleba Mkoani Kagera wametakiwa kujitambua na kubadilika ili kuleta maendeleo na kujenga dini kwa misingi ya imani.

Hayo yamebainishwa na Sheikh wa wilaya ya Muleba Sheikh Zakaria Mussa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid el Fitri ambapo kiwilaya limefanyika hapo jana june 16,2018 katika kata ya kishanda.


Sheikh Zakaria amesema kuwa viongozi wengi wamekuwa na ushirikiano mdogo kwenye kujenga dini hiyo hivyo ni wajibu wa kila kiongozi kutambua majukumu yake ili kuendana na hali ya sasa.


Awali akisoma Risala kwa mgeni rasmi Imamu wa Msikiti wa Ijumaa Kishanda namba mbili , Rajabu Rozzo ameomba waumini wa dini hiyo kushirikiana kwa ajili ya kujenga msikiti ambapo kwa sasa wana abudia kwenye jengo la muda.

 Aidha amesema kuwa inahitajika zaidi ya shilingi milioni 20 ili kujenga msikiti wa kudumu na waumini waliopo kwenye msikiti huo ni 501 wanaume 81 wanawake 105 na watoto 324.

 
 
 
 

Post a Comment

0 Comments