habari


Ujerumani Yatolewa katika Hatua ya Makundi ya Kombe la Dunia 2018.

Bingwa Mtetezi wa Kombe la Dunia 2014,Ujerumani imekosa kuutetea Ubingwa wake baada ya kuchapwa magoli 2-0 na Korea Kusini katika mchezo wa Kundi F June 27, 2018 wa Kombe la Dunia Uwanja wa Kazan Arena nchini Urusi.

Mabao yamefungwa na Kim Young-Gwon dakika ya 90+4 na Son Heung-Min dakika ya 90+7.

 
 
Hii ni mara ya kwanza ndani ya miaka 80 kwa Ujeruman kutolewa katika hatua ya makundi ya kombe la Dunia. 

Nayo Sweden imeichapa 3-0 Mexico, mabao ya Ludwig Augustinsson dakika ya  50, Andreas Granqvist kwa penalti dakika ya 62 na Edson Álvarez aliyejifunga dakika ya 74.

Mexico sasa inaungana na Sweden kwenda hatua ya 16 Bora na Watacheza kwa Brazil v Mexico na Sweden v Switzerland.

 

Post a Comment