habari


Selestini katibu wa chama cha watu wenye ulemavu Missenyi: Watu wenye ulemavu wapewe elimu ya ufundi ili wasiwe tegemezi.

MISSENYI: NA WILLIAM MPANJU
Watu wenye ulemavu Wilayani Missenyi mkoani  Kagera  wametakiwa kujifunza kazi za ufundi kulingana na ulemavu  walionao ili kuondokana na Maisha tegemezi katika jamii.

Akizungumza na mwandishi wetu Katibu wa chama cha watu wenye Ulemavu wilayani Missenyi mkoani Kagera Bw.Selestini Mkanadala amesema baadhi ya watu wenye ulemavu wamekuwa tegemezi jamba linalo wafanya kuendelea kuwa masiki katika maisha yao .

“Mimi nadhani sasa nijukumu la kila mtu mwenye ulemavu kuhakikisha anajifunza ufundi kulingana na hali aliyo nayo ili ajiajiri na kuondokana na maisha ya kuwa tegemezi”alisema Selestini.

Bw.Selestini Mkanadala ambaye ni mlemavu wa miguu  amesema njia pekee ya watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi nikufanyakazi kulingana na ulemavu wao walionao nakuwa dhambi kubwa katika maisha ni kukata tamaa.

Bw.Selestini ambaye ni katibu wa chama cha watu wenye ulemavu yeye anamiliki kalakana ya ufundi wa pikipiki ambapo anafanya kazi ya kubadilisha pikipiki  zenye magurudumu mawili nakuanza kutumia magurudumu matatu.

Hatahivyo Bw.Selestini amesema changamoto kubwa inayo wakabili watu wenyeulemavu niukosefu wa elimu nakuwa iwapo watatiwa elimu ya ufundi basi itawasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia kazi watakazo kuwa wakizifanya.

Post a Comment

0 Comments