habari Mpya


RC Kigoma –Wakimbizi Endelea kutumia Majiko Banifu na Gesi ili Kutoharibu Mazingira.

 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea  Ndagala akipokea Maelezo ya Mazao ya mboga mboga yanayo limwa na wakimbizi Kambi ya Nyarugusu katika mradi wa utunzaji wa Mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma,Kanali Hosea Ndagala  akioneshwa na Afisa wa Shirika la CEMDO majiko banifu yanayotumia kuni chache kwa lengo la kutokomeza uharibifu wa mazingira.

Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

Zaidi ya tani 160 za matumizi ya nishati ya  kuni na mkaa  hutumika katika  kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kwa siku moja, kwa  matumizi ya kupikia.

Hivyo hali ina sababisha uharibifu wa mazingira katika maeneo yaliyokaribu na kambi hizo.

Hayo yamebainishwa June 5,2018 wakati wa  kilele cha Maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ,  yaliyofanyika kimkoa katika Kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Akizungumza  Mratibu wa mradi wa utunzaji wa mazingira  kambini CEMDO Tanzania Frank Kayegameni akitoa taarifa ya mradi huo amesema kutokana na  idadi kubwa ya wakimbizi  kambi ya Nyarugusu ambayo imesababisha uhitaji mkubwa wa matumizi ya mazao ya misitu.

Amefafanuana  kuwa, Wakimbizi huenda kutafuta kuni nje ya kambi kwa kukata miti ambapo kwa siku inakadiriwa mtu mmoja anatumia kiasi cha kuni kilo moja na kambi inakadiriwa kuwa na wakimbizi 152,309 hivyo kusababisha  uharibifu mkubwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea  Ndagala akipokea Maelezo ya Mazao ya mboga mboga yanayo limwa na wakimbizi Kambi ya Nyarugusu katika mradi wa utunzaji wa Mazingira.

Amesema katika kupambana na hali hiyo Shirika la uhifadhi wa mazingira  na utunzaji wa mazingira kambini ( CEMDO) Tanzania,  kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameandaa utaratibu wa upandaji wa miti 1,425,223  katika Vijiji 13 vinavyozunguka Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kwa mwaka 2017/2018 , kugawa majiko banifu kwa kaya 9600 za wakimbizi.

Pamoja na majaribio ya ugawaji wa gesi  kwa kaya 3180 lengo likiwa ni kupunguza matumizi ya nishati ya mkaa na kuni  yanayosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira pamoja na  kuboresha mazingira kutokana na uharibifu mkubwa wa uoto wa asili  unaotokana na ukataji miti ovyo. 
Mmoja wa Wakimbizi akimuelezea Mkuu wa Wilaya namna wanavyo yatumia Majiko Banifu kuhakikisha hawaharibu Mazingira.

Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema  kauli mbiu ya maadhimisho ya mazingira ni "MKAA NI GHARAMA; TUMIA NISHATI MBADALA",Ambapo amesema kauli hiyo inasaidia utunzaji wa misitu na mazingira, lakini kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakimbizi kupewa majiko banifu na gesi kwenda  kuuza kwa Watanzania ilikujipatia fedha na kuendelea kuharibu mazingira na kuwataka wakimbizi kuacha tabia hiyo na kuendelea kutumia majiko yaliyotolewa na shirika hilo.

Naye Rais wa Wakimbizi Kambi ya Nyarugusu  Abilola Angelique amesema wao kama wakimbizi hawana budi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na mashirika yanayo wahudumia, kwa kuwa wanapotunza mazingira hata wao wanaendelea kunufaika kwani watatumia ardhi hiyo kulima mazao ya mboga mboga kwa ajili ya kujikimu na watoto wao.

Amewaomba wakimbizi wenzake kuendelea kusimamia utunzaji wa mazingira.

Post a Comment

0 Comments