habari Mpya


Radio Kwizera FM Yatua Jijini Mwanza (97.7 fm).

Kituo cha Utangazaji cha RADIO KWIZERA FMkilichopo wilayani Ngara mkoani Kagera katika kuhakikisha kinaenda na mpango wa kuongeza wigo wa usikivu , imewasha rasmi masafa yake May 30,2018 Jijini Mwanza ambapo inasikika kupitia masafa ya 97.7 fm.  

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa RADIO KWIZERA Padri.Damas Missanga amsema kuwa Kuanza kusikika kwa matangazo ya kituo hicho Jiji la Mwanza na maeneo Jirani kupitia 97.7 fm ni kuangalia Uhitaji na Maendeleo ya Jamii katika kuhabarisha, kuburudisha pamoja na kuelimisha.
 
Aidha, RADIO KWIZERA  kwa sasa inasikika NGARA 97.9 fm,BUKOBA 97.7 fm,KIBONDO 93.6 fm, KASULU na KIGOMA 94.2 fm,KAHAMA 97.3 fm, GEITA 90.5 fm inazidi kuishukuru Serikali na Wadau wake wote hususani wasikilizaji wake kwa kuendelea kuwaunga mkono pamoja na kuwaahidi wasikilizaji katika mkoa wa Mara/Musoma kuwasha Matangazo yake hivi karibuni ili kuhakikisha wanapata matangazo yake.

Post a Comment

0 Comments