habari


Mradi wa maji ulioanza kutekelezwa 2013 wilayani Ngara kwa kutengewa milioni 700 mpakasasa haija kamilika.

Pichani ni Diwani wa Kata ya Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera Bw.Hamisi Baliyanga.
Picha na story Shaaban Ndyamukama
Mradi wa kilimo cha Umwagiliaji katika bonde la mto Bigombo kata ya Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera, ulioanza kujengwa kuanzia mwaka 2013 kwa kutengewa shilingi milioni 700 haujaanza kutekelezwa na wananchi kuiomba serikali kuongeza fedha ili uweze kuwanufaisha.

Diwani wa kata ya Rulenge wilayani Ngara Bw Hamisi Baliyanga altoa ushauri huo baada ya kutembelea mradi huo jana  eneo la Goyagoya ambao ulijengewa kuta za kuhifadhi maji kwa ajili ya kilimo  na sehemu ya kunyweshea mifugo ya kata hiyo
Bw Baliyanga alisema mradi huo ulilengewa Shilingi milioni 700 na kunufaisha wananchi 450 kwa  kulima mazao ya chakula na biashara zikiwemo bustani za mazao ya aina mbali mbali kuongeza lishe na hata mazao kuwa ya kibiashara

Alisema yalishatengwa maeneo ya kilimo kwa wenye kuhitaji ardhi kujiandaa kuzalisha mazao lakini hawapati mrejesho kueleza changamoto zilizojitokeza na kwamba baadhi ya miundombinu iliyowekwa kwenye mradi huo imeanza kuharibika

Alisema mkandarasi aliweka mabunio ya kutekeleza mradi huo kwa kujichanganya na fedha iliyotengwa haikukidhi mipango ya kujenga miundombinu iliyohitajika na sasa unalalamikiwa na wananchi kwamba umetelekezwa.
"Wametembelea mawaziri wa kilimo na umwagiliaji na wakuu wa wilaya lakini hakuna kinachoendelea na ungeweza kunufaisha wanachi wakari huu wa kiangazi" Alisema
Alisema wananchi walikuwa na matarajio makubwa ya uzalishaji wa mpunga viazi vitamu mahindi na magimbi kwa kipindi cha kiangazi baada ya kukamilika mradi huo ambao serikali imeutelekeza.
Pichachani ni Afisa kilimo wilayani Ngara mkoani Kagera Costantine Mudende.
Hata hivyo Afisa Kilimo wilayani Ngara Costantine Mudende amesema changamoto iliyopo katika mradi huo ni uhaba wa fedha kutoka wizara ya kilimo na umwagiliaji  na kwamba mara fedha zikipatikana mradi huo utatekelezwa.


Post a Comment

0 Comments