habari


Mkuu wa Mkoa Kigoma apiga marufuku vitendo vya uchomaji Moto Misitu.

KASULU: NA ADRIANI EUSTACE 

Kaimu mkuu wa mkoa wa kigoma ambae ni mkuu wa wilaya ya Kibondo Bw.Louis Peter Bura amepiga marufuku vitendo vya uchomaji moto misitu, wizi wa miti na kukata miti ovyo badalayake wananchi wafuate ushauri unaotolewa na wataalamu wa kilimo kutokana na wakulima wengi kuandaa mashamba yao kienyeji na kupelekea kuharibu mazingira.

Bw.Bura ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi, viongozi na wadau wasimamizi wa mradi wa upandaji miti uliozinduliwa katika kata ya Muhunga halimashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma akimuwakirisha mkuu wa mkoa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga.
Pichani aliye simama ni mkuu wa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma Louis Peter Bura akizungumza katika wakati wa zoezi la upandaji Miti 
Amesema mamlaka zinazohusika na kudhibiti vitendo vya uharibifu wa mazingira zichukue hatua dhidi ya wahusika pindi wanapobainika kwakua maeneo mengi ya mkoa wa Kigoma huo yanaharibika hasa katika kipindi cha uandaajiwa mashamba kwa wakulima sambamba na kiangazi ambapo wafugaji wengi hutafuta malisho ya mifugo Yao.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa upandaji miti kutoka katika kampani ya Aliance One Bw.Benjamini Mangu amesema licha ya juhudi zinazofanywa na kampani hiyo katika kulinda mazingira,uwepo wa migogoro mingi ya radhi, uchomaji ovyo misitu na wizi wa miti ni changamoto kubwa zinazokwamisha utekelezaji wa mradi huo na kwamba serikali kutakiwa kuchukua hatua Za kisheria pindi wanapobainika.

Pichani juu na chini ni muonekano wa baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa upandaji Miti wakifuatia hotuba iliyokuwa ikitolewa na mkuu wa wilaya ya Kibondo Louis Peter Bura ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo.
Post a Comment

0 Comments