habari Mpya


Milioni 22 za Mfuko wa Jimbo zatumika Kuchochea Miradi ya Wananchi Ngara,Kagera.

Na-Shaaban Ndyamukama.

Jumla ya Shilingi milioni 22 za mfuko wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera zimetumika kuchochea miradi ya wananchi waliyoanzisha kwa ajili ya maendeleo ili kupunguza changamoto za maisha.

 Katibu wa Mbunge Jimbo la Ngara anayesimamia tarafa ya Rulenge na Murusagamba Bw Lengo Kapfusi amesema kati ya fedha hizo Shilingi milioni 12 zimetumika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu ya msingi na sekondari.

Taasisi nyingine zilizonufaika na fedha za jimbo tarafa ya Rulenge na Murusagamba ni Zahanati ya Nyarulama, Muyenzi , Keza, Ndomba na Murusagamba Sekondari kunako kuboresha miundombinu na mazingira ya kufundishia. 

Aidha Mbunge wa Jimbo la Ngara Alex Gashaza amethibitisha fedha hizo kutolewa na kwamba kwa mwaka wa fedha 2017/2018  Jimbo limepokea shilingi milioni 63 ambapo halmashauri imejiazima Shilingi milioni 28 ili kuandaa mpango mkakati wa maendeleo ya miaka mitatu.
Kikundi cha Walemavu Rulenge kilichopokea Shilingi milioni 2 na hapa wakionesha mbuzi walionunuliwa kutokana na kupokea Fedha za Mfuko wa Jimbo, benki wameweka Shilingi 300,000 na kiasi kingine wamekopeshana kwa riba ya asilimia 10 na kurejesha kila baada ya miezi mitatu. 

Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw Charles Kagambokabi anabainisha kuwa Jumla ya Mbuzi 11 wamenunuliwa na malengo ya kikundi hicho chenye wanachama 28 ni kufikisha mbuzi 25 na kwamba kikundi kimelenga kukopeshana, kupanda miti miche 5000 ambapo hadi sasa kimeuza miche 2000 sawa na Shilingi 200,000.

Post a Comment

0 Comments