habari


MELI YA MV UMOJA YA MIZIGO KUANZA RASMI SAFARI ZAKE MWANZA KWENDA UGANDA.

 MWANZA KOSTA KASISI
Shirika la Reli nchini TRC limezindua rasmi safari za kusafirisha mizigo ya contena kutoka jijini Dar es salaam, mwanza  hadi nchini Uganda kupitia bandari ya Mwanza kwa kutumia meli ya MV Umoja.

Akizungumza katika uzinduzi huo mkurugenzi wa TRC hapa nchini Masanja Kadogosa amesema kuwa mkakati wa shirika hilo ni kuhakikisha linaboresha huduma za usafirishaji wa mizigo inakuwa rahis na kwa gharama nafuu hali ambayo itachangia kukuza uchumi wa wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa.
Muonekano wa ndani wa Meli ya Mv Umoja. 
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa mwanza aliyekuwa mgrni rasmi amesema kuwa kuanza kwa safari hyo kumefungua njia ya kibiashara kati ya Tanzania na Uganda huku yakiwa ni matokeo ya viongozi wawili wa Tanzania na Uganda waliojadili na kuona namna ya kushirikiana katika usafirishaji

Shirika la Reli nchini TRC lilisitisha huduma ya usafirishaji was makontena kwa njia ya meli mwaka 2009 ambapo meli ya Mv umoja ndio ilikuwa ikitumika ambapo ni takriban miaka 9 bill meli hiyo kufanya kazi
Meli ya Mv umoja ilitengenezwa mwaka 1960 ikiwa na uwezo wa kubeba  makontena 19

Post a Comment

0 Comments