habari


MAGARI YA MIZIGO ZAIDI YA 60 YAZUIWA MPAKANI MWA MTUKULA MKOANI KAGERA KUINGIA NCHINI UGANDA

MISENYI. Na Shaaban Ndyamukama
Magari 60 ya mizigo ya mchele kutoka Tanzania yameendelea kuzuiliwa mpakani mwa Mtukula  mkoani Kagera kuingia nchini Uganda baada ya wafanyabiashara wa nchi hiyo  kushindwa kulipia ushuru mamlaka ya mapato ya Uganda URA.

Afisa wa mamlaka ya mapato TRA mkoani Kagera  Adamu Ntago alisema  magari hayo yenye   vitunguu na mchele yaliruzuiliwa kwenda nchini Uganda kupeleka bidhaa hizo kwa wateja wake baada ya kuwepo ongezeko la ushuru nchini humo.

Ntago alisema mgogoro wa ushuru kwa wafanyabiashara hao katika mpaka wa Mtukula utapatiwa ufumbuzi baada ya  kufikishwa wizara ya kilimo na fedha upande wa Tanzania na  viongozi ngazi ya juu wanafanya mipango ya kukutana .

Alisema ushuru huo unawaumiza wafanyabiashara wa Tanzania kwa kushindwa kuuza bidhaa zao kama mchele na vitunguu wakipitia njia za nchi kavu baada ya kupandishiwa ushuru wa asilimia 75 tofauti na wanaopitia bandari ya Mwanza.   
Wiki iliyopita magari hayo yalizuiliwa na mamlaka ya mapato ya Uganda URA  baada ya  kupandisha ushuru wa mchele kwa  tani 30 kulipia Sh8 milioni kutoka Sh4 milioni ambapo kwa Uganda ilikuwa  Sh6 milioni  ikifikia Sh10 milioni 

Mkuu wa wilaya ya Misenyi mkoani Kagera Dennis Mwila alisema   magari hayo yenye   vitunguu na mchele yaliruzuiliwa kwenda nchini Uganda kupeleka bidhaa hizo kwa wateja wake baada ya kuwepo ongezeko la ushuru nchini humo.

Kaanali Mwila Mwila alisema kinachosubiriwa  ni viongozi wenye mamlaka kutoka  wilaya ya Misenyi mkoani Kagera na  Kiyotela nchini Uganda kuweka utaratibu na kuridhia ushuru ambao hautaumiza wafanyabiashara wa pande mbili
Alisema Vitunguu kwa semi tela la tani 30 ilikuwa Sh60,000 mpaka Sh400,000 za kitanzani au kutoka Sh100,000 mpaka Sh600,000 za Uganda na kwamba ushuru huo umekiuka makubaliano ya  Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC)

"Viongozi wa wilaya hizi jirani tunawasiliana na mamlaka zilizo juu yetu kufanya majadiliano kuondoa tatizo na kuwaruhusu wafanya biashara wetu kuendelea na safari zao kuepuka bidhaa zao kuharibika ndani ya magari" Alisema DC Mwila

Alisema kutokana na ushuru wa mchele na vitunguu kutapanda nchini Uganda na kushuka Tanzania  baada ya nchi yetu wiki  mbili zilizopita  kupandisha ushuru   maharage, Mafuta ya kupikia aina ya Mkwano, sukari pamoja na mahindi.

Hata hivyo  alisema hali ya ulinzi na usalama katika mpaka wa Mtukula  ni nzuri na mazingira  yanaridhisha  hivyo madereva wasubirie vikao na maamuzi ya viongozi wa pande mbili za nchi na kupewa taarifa za kuendelea  na safari yao. 


Post a Comment

0 Comments