habari Mpya


Kitoto Cha Miezi Sita Chatupwa Kichakani,Mabawe,Ngara Kikiwakimefariki.

Wananchi wakitazama Mfuko unaosadikiwa kuwemo Kitoto Kichanga.

Picha/Habari Na Mohamed Makonda.

Mtoto mchanga anaekadiriwa kuwa na umri wa miezi sita amekutwa ametupwa akiwa tayari amefariki kwenye mfuko wa kubebea nguo leo June 5, 2018 katika Kijiji cha Muweza,Kata ya Mabawe Wilayani Ngara Mkoanai Kagera.

Akizungumza na Radio Kwizera FM, Mtendaji wa Kata ya Mabawe Bw Jonas Gwassa amesema amepokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa raia wema ambapo baada ya kufika eneo la tukio amekuta mfuko huo na alipo ufungua akaona mtoto huyo akiwa amefariki.

Mfuko unaosadikiwa kuwemo Kitoto Kichanga.


Bw.Gwassa ameeleza kwamba ametoa taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Kabanga lakini mpaka Radio Kwizera inaondoka katika eneo la tukio walikuwa hawajafika. 

Baadhi ya Wananchi waliofika katika eneo hilo wamelaani kitendo hicho na kuwa ni kitendo cha kinyama huku wakiwataka vyombo vya usalama kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakaye bainika kuwa amefanya tendo hilo.

Hata hivyo jeshi la polisi Wilayani Ngara limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi unaenedelea kubaini muhusika wake.

Post a Comment

0 Comments