habari Mpya


Kamati ya Siasa Mkoa wa Kagera Yatembelea na Kukagua Miradi ya Maendeleo Muleba.

Na Lucy Binamungu –Muleba.

Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kagera ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Bi. Constancia Buhiye imetembelea na kukagua miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015.

Ziara imeanzia kwenye mradi wa Maji Katoke ambapo changamoto mbalimbali zimetolewa na wananchi kuwa mradi haufanyi kazi na hautoi maji, maji yakifunguliwa mabomba yanapasuka, tanki linavuja na tayari mkandarasi amekamilisha kazi na kuondoka.

Akifafanua juu ya changamoto hizo Mhandisi wa Maji (w) Boniface Lukoo ameeleza kuwa ni kweli mradi umekamilika na upo chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja.

Sababu kubwa ya matatizo haya ni kutokana na mradi ulivyosanifiwa.
Mhandisi Mshauri alivyasanifu baadhi ya vitu havikuzingatiwa ikiwemo miinuko (heads) makadilio hayakuwa sahihi. Pia hali inayopelekea maji yanapofunguliwa mabomba kupasuka ni kutokana na upepo ulio kwenye mabomba.

Aidha, mradi kutofanya kazi ni kutokana na Kamati ya Maji ya Kijiji kutofungulia maji kutoka kwenye chanzo kuja kwenye tanki na kisha kuyasambaza kwa wananchi hivyo wananchi kukosa maji. 

Ujenzi wa Daraja la Kishara wilayani Muleba mkoani Kagera ukiendelea.Picha Na Lucy Binamungu –Muleba.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Bi. Constancia Buhiye amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Emmanuel Sherembi kusimamia na kuhakikisha mapungufu yote yaliyobainishwa na wananchi yanafanyiwa kazi na kukamilika ndani ya miezi 6.

Nae mlezi wa mradi huo ahamie kwenye eneo la mradi huo mpaka mapungufu yatakapokamilika.

Katika ziara hiyo, Kamati ya Siasa ya Wilaya itatembelea na kukagua Ujenzi wa Mradi wa Daraja la Kishara, Mradi wa Umwagiliaji Buhangaza na Buyaga.

Tenki laMaji la Maradi wa Maji Katoke, wilayani Muleba mkoani Kagera.

Viongozi mbalimbali wa Serikali na Kamati ya Siasa Mkoa wa Kagera na wilaya ya Muleba ambapo ikiwa wilayani humo itatembelea na kukagua Ujenzi wa Mradi wa Daraja la Kishara, Mradi wa Umwagiliaji Buhangaza na Buyaga.


Post a Comment

0 Comments