habari


KAMACHUMU STANDY UNITED WATWAA NG,OMBE 1 BAADA YA KUWATANDIKA BIRABO FC BAO 2-1

Muleba na Shafiru Yusufu
Timu  ya kamachumu standy united  imejinyakulia ng’ombe Mnyama baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa  1 dhidi ya timu ya Birabo fc katika ligi  ya jamii cup iliyochezwa jana kwenye uwanja wa shule ya msingi NShamba Tapa wilayani Muleba Mkoani Kagera.

Akikabidhi zawadi kwa washindi wa ligi hiyo Diwan wa kata ya Karambi Bw.Felix France  ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema mshindi wa kwanza amejinyakulia Ng’ombe mmoja Mwenye thamani ya shilingi laki nane mshindi wa pili Ngombe Mwenye thamani ya laki sita huku mshindi wa tatu amejinyakulia mbuzi 1 mnyama.

Aidha amewataka wachezaji pamoja na mashabiki kucheza Michezo yenyetija katika jamii kwani serikali inashirikiana nao ili kuinua vipaji vya wachezaji.

Nao manahodha wa timu zote mbili wameshukuru mashabiki pamoja na wadau mbali mbali wa Michezo kwa ushirikiano wa waliouonesha mpaka kufikia tamati ya ligi hiyo.
Hata hivyo mshindi wa kwanza  ni kamachumu stand united mshindi wa pili ni Birabo FC na mshindi wa tatu ni NShamba Stars.


Post a Comment

0 Comments