habari Mpya


KAGERA-Wahukumiwa Kifo kwa kumuua Mtoto wa Kambo.

Na-James Jovin -Radio Kwizera -Biharamulo.

Mahakama kuu Kanda ya Bukoba iliyokaa June 01, 2018 Wilayani Biaharamulo Mkoani Kagera imewahukumu kifo wakazi wanne wa wilaya ya Ngara baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya mauaji. 

Haruna Shomari wakili wa Serikali mkoa wa Kagera mbele ya Jaji Salumu Bongore amesema kuwa waliokutwa na hatia katika kesi hiyo ni Aneth Furaha, Judith Robert, Edison Duguye na Shaban Rihege wakazi wa kijiji cha Kabanga Wilayani Ngara.  

Amesema mnamo tarehe 20, July mwaka 2013 katika kijiji cha Kabanga kata ya Kabanga Wilayani Ngara watuhumiwa wote kwa pamoja walishiriki kumuua.

 Marehemu Shaban Furaha Salamu kwa makusudi kisa ikiwa ni maelewano mabaya na mama yake wa kambo ambaye ni Aneth Furaha aliyetaka mtoto wake wa kambo auwawe ili aweze kuishi kwa amani.  

Baada ya vielelezo vyote kuonesha kuwa watuhumiwa walitenda kosa hilo mahakama kuu imeweza kuwatia hatiani ambapo Jaji Salumu Bongore ametoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojichukulia sheria mkononi ya kuua raia wasio na hatia.

Post a Comment

0 Comments