habari Mpya


Idara ya Elimu Ngara Yaadhimisha Kilele cha Wiki ya Elimu kwa Kuhamasisha Taaluma.

Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kupitia Idara ya Elimu Msingi, imetumia Maadhimisho ya Wiki ya Elimu kuhamasisha Jamii kutambua umuhimu na kuongeza ari ya utendaji kazi kwa Walimu na Wanafunzi wilayani humo.
 Akisoma risala wakati wa maadhimisho hayo,kwa niaba ya Afisa Elimu Wilaya ya Ngara May 30,2018, Afisa Taaluma (W) Bw. Oswald Rujuba, amesema wameaitumia siku hiyo ili kuihamasisha Jamii kuinua taaluma ya Wanafunzi wilayani Ngara.

Amesema maadhimisho ya siku ya kilele cha Wiki ya Elimu yamesimamiwa na idara ya Elimu Msingi na Elimu Sekondari na kwamba idara ya Elimu Msingi katika wiki hiyo imefuatilia Maendeleo ya taaluma katika Sule ya za Msingi zipatazo 74.

Kutokana na hali ya taaluma wilayani kwetu kushuka; tumetoka nafasi ya Kwanza hadi ya Nane kimkoa, tuliamua kufanya maadhimisho haya kwa kutembelea shule moja, ili kuhamasisha na kuongeza ari ya utendajikazi kwa walimu na wanafunzi wajisomee kwa bidi.” Alisema Afisa Elimu Taaluma Bw. Rujuba.

Katika risala yake ameihamasisha Jamii, kuwekeza katika Elimu kama hatua muhimu ya kuzalisha nguvu kazi yenye ujuzi wa kulisaidia taifa lao, na kuongeza kwamba uhamasishaji huo, umepelekea ofisi yake kuongeza idadi ya Wanafunzi 84,125 waliosajiliwa.

Amefafanua kwamba idara ya msingi imefanya vizuri kitaaluma, ambapo katika mitihani ya darasa la VII kitaifa kwa miaka mitatu tangu mwaka 2015 hadi 2017, imekuwa ya kwanza kimkoa na imefanikiwa kuvuka lengo.

Maadhimisho ya siku ya kilele cha wiki ya Elimu wilayani Ngara yameabatana na kuwatunuku vyeti walimu wakuu, ambao shule zao zimefanya vizuri kitaaluma, ambapo shule tano za sekondari na tano za msingi wametunukiwa vyeti hivyo.

Idara ya Elimu Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara inazo shule 121, shule 115 ni za serikali, ambapo shule 06 ni za watu binafsi, na kwamba idara yake ina walimu 1,373; walimu wa kiume ni 867 na wa kike 506.

Post a Comment

0 Comments