habari Mpya


Hii ndio Sababu ya Umeme Kukatika Mara kwa Mara wilayani Karagwe.

Waziri wa Nishati wa Tanzania Bw.Medard Kalemani akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha katanda ,Kata ya Kihanga wilayani Karagwe mkoani Kagera June 11,2018 alipofika kwa ajili ya uzinduzi wa Umeme wa REA awamu ya III.

Picha /Habari Na Elen Magambo –Radio Kwizera –Karagwe.


Imeelezwa kuwa chanzo cha umeme kukatika mara kwa mara wilayani Karagwe Mkoani Kagera kunatokana na miundombinu ya umeme kuwa mibovu wilayani humo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nishati Bw.Merdadi Kalemani wakati akijibu swali la mbunge wa jimbo la Karagwe Bw Innocert Bashugwa ambaye alitaka kujua kwanini umeme unakatika mara kwa mara.
 
Bw Kalemani amesema sababu kubwa ya umeme kukatika ni kutokana na nguzo kuanguka pamoja Nyaya kugusa miti hivyo kwa sasa serikali imetenga bajeti kwa ajili ya kuboresha miundombinu hiyo kwa kila Mkoa.

Katika hatua nyingine amewataka Wananchi kutoa taarifa ofisi za shirika la umeme Tanzania TANESCO wanapobaini nguzo zinapodondoka ili kuweza kutatatua changamoto hiyo mara tu inapojitokeza.

Post a Comment

0 Comments