habari Mpya


Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga yatoa zaidi ya shilingi milioni 100 kwaajili ya Saccoss ya Vijana

Pichani ni mkuu wa mkoa Shinyanga Bi.Zaibabu Terack watatu kutoka kulia na Vijana wa mkoani humo CDT akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 105000,000 kwa vijana wa Saccoss mkoani humo.
Na mwandishi wetu Simon Dionizi 
Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga imetoa zaidi ya shilingi milioni 100 kwaajili ya Saccoss ya Vijana CDT ili kuendeleza miradi yao.

Akikabidhi fedha hizo mkuu wa Mkuu wa mkoa Shinyanga Bi.Zainabu Terack amesema kuwa serikali imedhamilia kuwainua vijana kiuchumi,hivyo vijana hao wanatakiwa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo itakayo wasaidia kuondokana na umasikini.
Serikali inadhamira yakwli ili kuwa saidia vijana kwakua ninyi ni Nguvu ya taifa hivyo kupitia pesa hii iliyotolewa na serikali vijana mnatakiwa kubuni miradi ya maendeleo ili kujikwamua kiuchumi”Amesema Bi.Terack
 
Pichani ni Mkuu wa mkoa Shinyanga Bi.Zainabu Terack akitembea kwaajili ya kukagua miradi ya maendeleo ya vijana.
Aidha mkuu wa mkoa Shinyanga Bi.Zainabu Terack amesema kuwa fedha hizo zinatakiwa kutumika kwa malengo yaliyo kusudiwa  ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa vijana wao katika vikundi.
Niwaombe viongozi wa Saccoss hii fedha zitumike katika malengo yaliyo kusudiwa lakini pia mkopo itolewe kwajina walio katika vikundi vya uzalishaji mali”Amesema Bi.Zainabu Terack.


Post a Comment

0 Comments