habari Mpya


Halmashauri ya Biharamulo Mkoani Kagera yatakiwa Kukamilisha Mradi wa Maji wa Bisibo na Kuukabidhi kwa Wananchi.

Na James Jovin –radio Kwizera Biharamulo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera Bi Konstansia Buhiye ameitaka halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kuhakikisha inakamilisha na kukabidhi mradi wa maji uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 300,kwa Wananchi wa Kata ya Bisibo uliokwama kwa zaidi ya Miezi mitano sasa. 

 Bi Konstansia ametoa kauli hiyo akiwa ziarani na Kamati ya Siasa ya Mkoa katika kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Kagera ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ambapo wilayani Biharamulo imetembelea mradi wa maji wa kijiji hicho uliogharamiwa na serikali kupitia program ya maendeleo ya sekta ya maji kwa ufadhili wa benki ya dunia .

Aidha ameitaka idara ya maji wilayani humo kutatua changamoto mbali mbali zinazokwamisha mradi huo ikiwemo kupasuka kwa mabomba, kuhakikisha maji yanatoka katika magati yote na kuelimisha wananchi umuhimu wa kuchangia huduma ya maji.

Kwa upande wake Bi Aquilina Martin akimwakilisha Mhandisi wa maji Wilaya ya Biharamulo amesema mradi huo utakapoanza kufanya kazi utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza upatikanaji wa huduma za maji kwa wanakijiji.

Post a Comment

0 Comments