habari


DC NGARA:VIJANA JITOKEZENI KWAWINGI MSHIRIKI MAFUNZO YA MGAMBO.


Pichani ni wanafunzi wa Jeshi la akiba Mgambo wakati wa uzinduzi  
NGARA: NA MWANDISHI WETU FADHILI KIJANJALI.

Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele amewata vijana wilayani Ngara kijitokeze kwa wingi kushiriki katika mafunzo ya mgomb.
Akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya Jeshi la akiba Mgambo wilayani Ngara mkoani Kagera yaliyo fanyika katika uwanja wa shule ya msingi Kumuyange kijiji cha Kumuyange wilayani.

Pichani aliye simama ni mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele. 
“Niwaombe vijana mjitokeze kwa wingi kujiunga na mafunzo ya Mgambo ili ya wasaidie kudumisha ulinzi na usalama katika maeneo yetu lakini pia nisehemu ya kujipatia jira”Amesema Mtenjele
Katika hafla fupi ya ufunguzi huo wa mafunzo ya Jeshi la Akiba amesema kwa sasa serikali wakati wakutoa ajira mbali mbali inatoa vipaumbele kwanza kwavijana wenye mafunzo ya mgambo.
“Napenda niwambie Vijana itumie hii fursa ya kujiunga na mafunzo ya Mgambo kwani kwasasa serikali wakati wa kutoa ajiri kwanza kabisa wanatoa kwa vijana walio hitimu mafunzo ya Mgambo hakuna sababu ya kuyakimbia mafunzo hayo kwani nikwa faida yenu wenyewe”amesema Mtenjele.

Amesema mbali na suala la ajira umuhimu wa mafunzo ya mgambo ni kuwapa vijana uzalendo lakini pia ni sehemu yakuimarisha ulinzi na usalama wa nchi na maeneo yao.

Kwa upande wake mshauri wa Mmgambo wilayani Ngaramkoani Kagera Afisa Mteule Agustino Tibamanya amesema changamoto kubwa wanayokumbana nayo wakati wa mafunzo ni idadi ndogo ya watoto wa kike wanaojiunga na mafunzo hayo.

Amsema mafunzo hayo ya Jeshi la akiba wilayani humo kwasasa linajumla ya wanafunzi 91 kati yao wakiume 88 wakike 3.

Post a Comment

0 Comments