habari Mpya


DC Ngara –‘’Toeni Elimu ya Mazingira Kuepusha Uaribifu Zaidi’’.

Picha /Habari Na-Mohamed Makonda.

Wataalamu na wadau wote wa mazingira katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera  wametakiwa kuendelea kutoa elimu ya mazingira, ili kuepeusha madhara yanayoweza kutokea kutokana na kukata miti hovyo, kuchoma misitu na kuharibu vyanzo vya maji.

Akiongea na Wananchi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Rulenge, wakati wa siku ya kilele cha wiki ya Mazingira Duniani June 05, 2018, kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, Afisa Tarafa wa Tarafa ya Rulenge Bw.Moris Mombia, amewataka wananchi kuwa na tabia ya kutunza mazingira.

Tunaharibu vyanzo vya maji, uonto wa asili matokeo yake; maji yatakauka, miti itaisha tutakuwa na jangwa, kwa hiyo hata huo mkaa hamtauchoma, matanuru ya matofari mtakosa kuni za kuchomea tofari, na wala maji ya kufyatulia tofari’’ Alisema Bw. Moris.

Amewataka Wananchi wa Ngara kuacha kabisa kutumia miti ya asili kuchomea mkaa, badala yake watumie miti ya kupanda kama vile mikalitusi na pine, huku akiwasisitiza kupanda miti kila wanapokata mti  kwa ajali ya matumizi ya kuchoma mkaa.

Naye Kaimu Afisa Usafi na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Bw.Zawadi Waziri, amewaambia Wananchi wanaojishughulisha na uchimbaji wa mchanga, kuchoma tofari na mkaa kujiunga katika vikundi ili waweze kupata leseni zitakazowasaidia kutambulike kisheria.

Amewataka kutumia nishati mbadala kama vile gesi, na majiko ya kisasa kwa ajili ya kuzuia uharibufu zaidi wa mazingira.

Wiki ya mazinigira imehitimishwa rasmi June 05, 2018, katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Rulenge, kwa kufanya usafi katika hospitali ya Rulenge, kutoa elimu ya mazingira kwa wachoma mkaa, wachoma tofari, wachimba mchanga na mama lishe.

Post a Comment

0 Comments