habari


DC KYERWA: NITADILI NA WAFANYA BIASHARABINAFSI WATAKAO NUNU KAHAWA KWA WAKULIMA.


KYERWA NA MWANDISHI WETU KAMALIZA JULIUS
Mkuu wa wilaya ya Kyerw mkoani Kgera Kanal Shaaban Lissu ampiga marufuku wafanya biashara binafsi wanao nunua zao la Kahawa kwa Wakulima nakuwa mfanya biashara binafisi atakae bainika akinunua zao hilo kwa wakulima atachukuliwa hatua za kisheria.

Amesema hayo katika zaoezi la kuwafungulia  account katika simu za mkononi wakulima wa zao la kahawa wilayani Kyerwa mkoani Kagera ili kuwarahisishia kupokea fedha zao kwa wakati pale wanapo uza zao hilo la katika Vyama vya Ushirika.

Kanali Lissu amesema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona wakulima wasio na Account za Bank wakipata usumbufu wakupata fedha za malipo ya zao lao la kahawa wapo uza ili kuondoa changamoto ya kulima hao kuchelewa kupokea fedha nakuwa ni vyema utumike utaratibu wa kuwalipa kupitia simu za mkononi.
 Tunawafungulia Account kupitia simu zenu za mkononi ili mpokee fedha zenu kwa wakati mnapo uza Kahawa yenu kwenye vyama vya ushirika lakini pia niwaombe wakulima msikubali kuwauzia Kahawa yenu wafanya biashara binafsi kwani mnapunjwa”alisema Kanali Lissu.

Kanali Lissu amesema wakulima wamekuwa wakiendelea kuwa masikini huku wakiwanufaisha wafanya biashara binafsi kwakuwa wafanya biashara hao hununua kwabei ambayo haimpi faida mkulima.

Kwaupande wao wakulima walio fungua Account za kiedha kupitia simu za mkononi wamempongeaza mkuu wa wilaya hiyo kwa hatua hiyo kwani itawasidia wao kupata fedha hizo kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments