habari Mpya


DC Kahama-‘’Mwananchi anetupa Mfuko wa Plastiki hovyo Kufikishwa Mahakamani’’.

Mrundikano wa Taka za Mifuko ya Plastiki –Picha Na Maktaba yetu.

Na Simon Dioniz –Radio Kwizera Kahama.

 Serikali Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga inatarajia kutumia Jeshi la akiba la Mgambo kukabiliana na Watu wanaotupa hovyo Mifuko ya Plastiki kama njia ya kutekeleza Sheria ya Mamlaka ya hifadhi ya Mazingira ya mwaka 2017.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Bw Fadhil Nkurlu wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake na kwamba wale watakaokamatwa wakitupa  taka hovyo watafikishwa mahakamani.
 
Amesema mamlaka ya Hifadhi ya Mazingira NEMC wametoa waraka wao wa kuzuia matumizi ya mifuko ya prastiki lakini watu wanaendelea kutumia mifuko hiyo kinyume cha sheria. 

 
Licha ya Serikali kupiga marufuku Utumiaji wa Mifuko ya Plastiki ,bado mifuko hiyo inatumiwa na Wafanyabiashara Sokoni.

Nao Baadhi ya Wakazi wa mji wa Kahama wameitaka halmashauri ya mji wa Kahama kuweka vitu vya kutunzia taka mitaani ambapo wamesema vifaa walivyopewa na kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA Buzwagi wamevitelekeza ofisini badala ya kuvisambaza kwenye mitaa ya mji huo  ili vitumike kutunzia taka.

Post a Comment

0 Comments