habari


DC Bukoba afanya ziara ya kushitukiza katika kiwanda cha kukoboa kahawa BUKOP Bukoba manispaa nakutoa maagizo haya.

Wapili pichani  kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Bukoba Manispaa mkoani Kagera Deodatus Kinawilo. 
BUKOBA:NA ANORD KAILEMBO.

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo afanya ziara ya Kushtukiza kwenye kiwanda cha kukoboa Kahawa cha BUKOP kilichopo manispaa ya Bukoba na kukiagiza chama kikuu cha Ushirika mkoani Kagera KCU kuweka usimamizi wa kutosha kwa wakulima ili kuondoa tabia iliyotajwa na wasimamizi wa kiwanda hicho ya kuchanganya mawe, mchanga na takataka kwenye kahawa.

“Niwaombe viongozi wa chama kihi cha ushirika kuweka usimamizi wa hali ya juu ilikudhibiti tabia za baadhi ya wakulima kuchanganya mawe na mchanga kwenye kahawa”alisema Kinawilo

Uongozi wa kiwanda hicho cha Bukop umesema wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa hasa wakulima kuchanganya mawe,mchanga na taka.

Katika utafiti uliofanywa na BUKOP kwa Gari moja lililokuwa na kilo elfu 10 na mia 4, walipata mapepe kilo 97, Mawe kilo 12, Taka kilo 2,  Mchanga kilo 4.

Pichani ni Kiwanda cha kukoboa Kahawa BukopPost a Comment

0 Comments