habari Mpya


AGONGA NYUMBA USIKU WA SAA TISA AKIENDESHA GARI AKIWA AMELEWA WILAYANI NGARA.

NGARA NA SHAABAN NDYAMUKAMA
Gari aina ya probox lenye namba za usajili T624CUN Limeacha njia na kugonga nyumba moja wilayani Ngara mkoani Kagera.

Tukio hilo limetokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Ngara mjini.

Chanzo cha habari kimeeleza kuwa ajali hiyo imetokana na Dereva wa gari hilo Bw. ADRIANI OSWARD kuendesha akiwa amelewa hali iliyo pelekea kuacha njia njia na kugonga nyumbahiyo ya Bw.Massen Saidy na kuvunja dirisha la nyumba ambapo mpaka sasa thamani ya vitu vilivyo haribika haijajulikana.

Hatahivyo dereva wa gari hilo anashikiriwa na Jeshi la polisi kwa uchunguzi na mahojiano zaidiPost a Comment

0 Comments