habari


AFARIKI KWAKUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA WATU WASIO JULIKANA

Pichani ni Baadhi ya mashuhuda wakishudia mwanamke aliye fariki.
Namwandishi wetu James Jovin.
Mwanamke mkazi wa kitongoji cha Nyakatuntu  Kanywamaizi katika mamlaka ya mji mdogo wa Biharamulo mkoani Kagera amefariki baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na watu ambao hawajafahamika mara moja.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyakatuntu kanywamaizi  Bw. Abraham Berenatus  ameiambia website hii kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo June 18, 2018 na aliyeuwawa ni Bi.Esteria John anayekadiriwa kuwa na miaka 50 mkazi wa kitongoji cha Nyakatuntu kanywamaizi

Bw.Berenatus amesema kuwa marehemu ni mzaliwa wa kijiji cha Kiruruma kata ya Bisibo katika kitongoji cha Nyakatuntu Kanywamaizi alikuwa akiishi kama mpangaji, ambapo hata hivyo haijabainika wazi sababu za kuuwawa kwa marehemu na waliotekeleza mauaji hayo hawajafahamika mara moja.

Bi.Ester josephat na Rajabu Nasibu ni miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni majirani na Nyumba aliyokuwa akiishi Marehemu, wanasema waliamka asubuhi na kukuta mwili wa marehemu ukiowa kando kidogo ya bara bara.

Pichani ni Mwili wa marehemu ukiwa umefunikwa kwenye shamba la Migomba.
Hata hivyo marehemu hakuwa na chuki wala tatizo na mtu yeyote na hawajabaini aliyefanya tukio hilo.
 
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bisibo Bw.Festo Mtatembwa amewataja wananchi kuacha kujichkukulia sheria mkononi bali iwapo wanamatatizo wafuate sheria ili kumaliza migogoro katika njia ambayo inakubalika hata mbele za mungu.

Jeshi la polisi wilayani Biharamulo limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo limefika eneo la tukio na kuruhusu mwili wa marehemu uzikwe..

Hata hivyo upelelezi zaidi wa tukio hilo unaendelea ili kuweza kujua sababu za kifo hicho na  kuwabaini wote waliohusika ili wachukuliwe hatua za kisheria .

Post a Comment

0 Comments