habari Mpya


Wilaya ya Sengerema Yagawa Vitabu 65,532 Kumaliza Uhaba wa Vitabu Darasa la Kwanza hadi la Tatu.

Na Erick Ezekiel –Radio Kwizera –SENGEREMA.

Jumla ya Vitabu 65,532 vyenye thamani ya Shilingi Milioni 393 vimetolewa na Halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza
ili kumaliza chnagamoto ya uhaba wa vitabu kwa Wananfunzi wa darasa
la kwanza hadi darasa la tatu.

Akikabithi vitabu hivyo katika hafla fupi iliyofanyika Shule ya msingi
Pambalu ,Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bw.Emmanuel Kipole amesema kuwa
kutolewa kwa vitabu hivyo vitakavyosambazwa kwenye shule tisini na
nane za serikali ni mpango wa kuboresha elimu nchini.
Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Sengerema Bw.Oscar Kapinga amesema
kuwa baada ya vitabu hivyo kufika mashuleni walimu watapata nafasi
nzuri ya kuwafafanulia wanafunzi kwa kuwa kila mwanafunzi atakuwa na
kitabu chake.

hata hivyo, Katika taarifa iliyosomwa na Mwl.Tema Heri kwa niaba ya
Mkuu wa shule ya Msingi Pambalu Bi.Sundi Mussa kwa Mkuu wa wilaya ya
Sengerema imeeleza kuwa shule hiyo haijapokea kitabu hata kimoja cha
mtaala mpya wa darasa la nne  na kwamba ufundishaji katika darasa hilo
mpaka sasa ni wa kusua sua kutokana na kwamba mtaala unaotumika
kufundishia wanafunzi wa darasa la nne ni wa zamani ambao sasa
umepitwa na wakati.
 Mkuu wa wilaya hiyo Bw.Emmanuel Kipole amesema kuwa changamoto hiyo
inafahamika Serikalini na mkakati wa kuitatua na kuimaliza kabisa
unaendelea.

Imeelezwa kuwa kupatikana kwa vitabu vya darasa la
kwanza hadi la tatu kumemaliza kabisa changamoto ya wanafunzi sita
kutumia kitabu kimoja ambapo kwa sasa serikali imetimiza mpango wa
kitabu kimoja kutumika kwa mwanafunzi mmoja.

Post a Comment

0 Comments