habari Mpya


Waziri Jafo Azindua Miradi Mitatu ya Maendeleo na Kuleta Neema ya Hospitali Tatu za Wilaya Mkoani Kagera.

Na: Sylvester Raphael.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleimani Jafo aweka mawe ya msingi katika miradi miwili ya afya na kuzindua mradi mmoja wa elimu Mkoani Kagera ambapo miradi hiyo imetolewa fedha na Serikali kwa ajili ya kuboreshwa na kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Waziri Jafo mara baada ya kuwasili mkoani kagera Mei 11, 2018 alianza ziara yake Wilayani Karagwe ambapo alizindua miradi miwili, mradi wa ukarabati wa vyumba vya madarasa vitano ujenzi wa vyoo matundu manane na ujenzi wa chumba cha stoo katika Shule ya Msingi Ihembe shule iliyojenwa mwaka 1948 na ilikuwa haijawahi kufanyiwa ukarabati hadi mwaka 2017.
Waziri Jafo alizindua shule hiyo baada ya Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kutoa fedha jumla ya shilingi milioni 66 kufanya ukarabati katika shule hiyo ambayo ilikuwa na hali mbaya sana. 

Waziri Jafo aliridhia kutoa fedha hizo baada ya utembelea shule hiyo mwaka 2017 na kuona ubovu wa miundombinu ya shule hiyo.
Waziri Jafo alizindua shule hiyo baada ya Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kutoa fedha jumla ya shilingi milioni 66 kufanya ukarabati katika shule hiyo ambayo ilikuwa na hali mbaya sana. 

Waziri Jafo aliridhia kutoa fedha hizo baada ya utembelea shule hiyo mwaka 2017 na kuona ubovu wa miundombinu ya shule hiyo.

Aidh, katika hatua nyingine Waziri Jafo aliweka mawe ya msingi katika Kituo cha Afya cha Kayanga Wilayani Karagwe na Zahanati ya Maruku Wilayani Bukoba. 

Katika kituo cha Afya Kayanga Serikali ilitoa shilingi milioni 670.7  ikiwa milioni 170.7 zilitolewa na mfuko wa Maafa Mkoa wa Kagera baada ya Tetemeko la Ardhi kutokea Mkoani Kagera Septemba 10, 2016.

Fedha hizo milioni 170.7 zilikuwa za kujenga  wodi ya wazazi, chumba cha kuhifadhia maiti, na nyumba ya kuzalishia umeme. 

Vilevile Serikali ilitoa milioni 500 kwaajili ya kujenga Jengo la wagonjwa wa nje, Nyumba ya mganga , chumba cha upasuaji, wodi ya wanaume, jengo la utawala na njia za kutembelea ambapo kazi hizo zote zimekamilika kwa asilimia 95.

Akiongea na wananchi Waziri Jafo katika miradi hiyo aliyoweka mawe ya msingi na kuzindua alisema kuwa Mkoa wa Kagera una bahati ya kupata fedha za miradi ambapo katika mwaka wa fedha 2018/2019 Ofisi ya Rais TAMISEMI imetenga fedha bilioni 105 za kujenga hospitali za Wilaya nchi nzima na mkoa wa Kagera umepata bahati ya Hospitali tatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Wilaya ya Karagwe na Kyerwa.

Tangu uhuru nchi nzima ilikuwa na hospitali za Wilaya 77 tu hadi mwaka 2018 lakini sasa Serikali imetenga bilioni shilingi 105 kwa ajili ya kujenga Hospitali za Wilaya 67  nchi nzima na Kagera imepata hospitali tatu kama nilivyo taja hapo awali, haya ni mapinduzi makubwa katika Sekta ya Afya yatakayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano,” Alifafanua Waziri Jafo.

Pia Waziri Jafo alisema kuwa tanga uhuru hadi mwaka 2018 nchi ilikuwa na Vituo vya Afya 115 lakini sasa Serikali imeamua kujenga vituo vya afya na kufikia idadi ya 208 na vituo hivyo vimejengwa kisasa kwa kuzingatia kuwa huduma zote lazima zipatikane katika vituo hivyo hasa huduma za upasuaji wa akiana mama wajawazito.

Waziri Jafo aliwaagiza  Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuhakikisha wanatoa mikopo kwa vikundi vya akina mama na vijana bila riba kwani fedha hizo zinazotolewa zinakuwa zimekusanywa kutoka katika kodi za wananchi wenyewe.

Ziara ya Waziri Jafo itaendelea Mei 12, 2018 Katika Manispaa ya Bukoba na Halmashauri ya Bukoba Pamoja na Kamati ya Bunge katika Shule za Sekondari Nyakato na Ihungo zinazojengwa upya baada ya kuharibiwa na Tetemeko la Ardhi Septemba 10, 2016.


Post a Comment

0 Comments