habari Mpya


Wananchi waaswa Kumuenzi Mwalimu Kasuku Bilago ili kuleta Tija Katika Maendeleo.

Hatimaye Mwili wa Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mwalimu Kasuku Bilago umepumzishwa leo May 31, 2018 katika nyumba yake ya milele huko Kata ya Kasuga wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

Mwalimu Bilago alizaliwa Tarehe 2/2/1964 na amefariki akiwa Mbunge wa kuchaguliwa wa Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma ambapo alichaguliwa mwaka 2015.


Mwalimu Kasuku Bilago alifikwa na umauti wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jumamosi May 26, 2018,jijini Dar es Salaam. 

Katika Ibada ya Mazishi yake, Wananchi waaswa kumuenzi kwa mema aliyoyatenda wakati wa uhai wake ili kuleta tija katika maendeleo kwao na taifa kwa ujumla.

Picha Na Faraja Marko –Radio Kwizera Kakonko.


Post a Comment

0 Comments