habari Mpya


Wananchi wa Nyamiranda-Muleba wagoma kuchangia Ujenzi wa Ofisi mpaka Wasomewe Mapato na Matumizi.


Ubovu wa Jengo la Ofisi y'a kijiji cha Nyamiranda kilichopo Kata ya Kyebitembe wilayani  Muleba mkoani Kagera.Jengo hilo limeharibiwa na Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo. 


Picha/Habari Na-Shafiru Yusuf -Radio Kwizera MULEBA.

Jengo hilo limeshindwa kuboreshwa  baada ya Wananchi wa kijiji hicho kukataa kuchangia Uenzi wa ofisi hiyo mpaka  pale watakaposomewa mapato na matumizi ya kijiji hicho.

Wakiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika May 14, 2018 baada ya mtendaji wa kijiji hicho Bw. Mswadick Mohammed  kutoa ajenda hiyo mbele yao, na kueleza kuwa wanashindwa kutoa huduma kwa sasa kwa Wananchi hao mpaka pale watakapo changia ujenzi wa ofisi hiyo iliyoharibiwa na Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Muleba.

Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Damaseni Karoli  amesema Mtendaji akiyekuwepo hakukabidhi nyaraka za ofisi , hivyo amewataka Wananchi kuwa na subira  mpaka pale Mtendaji aliyekuwepo Bw. Brasio  Nzakumuha akabidhi nyaraka hizo.

Post a Comment

0 Comments