habari Mpya


Wana Kakonko wachangia Lita 58 za Damu kupitia Kampeni ya Damu yako,Maisha yangu ya Radio Kwizera.

Uniti za Damu zikia kwenye Chombo cha Kuhifadhiwa baada ya Kutolewa Jana May 12,2018 katika zoezi la Kampeni ya Radio Kwizera ya Uchangiaji Damu Salama.

 Na Shaaban Ndyamukama-Radio Kwizera.

Jumla ya lita 58 za damu zimepatikana katika wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma baada ya Wananchi kujitokeza kusaidia walioko katika vituo vya kutolea matibabu.

Akielezea zoezi la kuchangia damu salama katika zoezi hilo lililofanyika May 12, 2018 eneo la Parokia Mtakatifu Tereza Mjini Kakonko, mmoja wa watoa huduma katika zoezi hilo amesema wamekuja baada ya kuwepo uhamasishaji kupitia Radio Kwizera ya wilayani Ngara mkoani Kagera.

Mganga mkuu wa wilaya hiyo Dr Joseph Tutuba amesema mahitaji ya damu ni makubwa kwa wanawake wanaojifungua ,watoto wadogo chini ya miaka mitano na wenye kupatwa ajali ambapo mahitaji ya damu salama katika wilaya hiyo ni lita 180 ambazo kwa wastani katika siku zinatakiwa kuwepo lita 6.

Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kakonko Bw.Simon Mando amepongeza Radio Kwizera katika kujitokeza kuhamasisha jamii kuchangia damu Kupitia kampeni yake ya DAMU YAKO ,MAISHA YANGU.
Uchangiaji ukiendelea Kakonko May 12,2018.

Mgeni rasmi katika zoezi hilo alikuwa mkuu wa wilaya hiyo Luteni Kanali Hosea Ndagala ambaye baada ya kuhutubia wananchi na ameelezea furaha yake ya kupata kiwango hicho cha damu.

Takwimu zinaonesha uhamasishaji wananchi kujitokeza kuchangia damu zimepatikana mpaka sasa Jumla ya Lita 574 ikiwemo Kakonko Lita 58 kwa wilaya ziizoshiriki Kampeni hiyo kama Ngara Lita 204, Biharamulo Lita 209, Karagwe Lita 53, Bukoba Manispaa Lita 50 za mkoani Kagera na sasa Kampeni DAMU YAKO,MAISHA YANGU imehamia mkoani Kigoma.

Post a Comment

0 Comments