habari Mpya


Vikundi 27 Wilayani Muleba Vyajengewa Uwezo Kuhusu Usimamizi Fedha na Rasirimali Watu.

Vikundi 27 vya Wanawake, Vijana na Walemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera,vimepewa elimu na kujengewa uwezo katika maswala ya rasilimali watu na usimamizi wa fedha.

  Habari Na-Shafiru Yusuf- Radio Kwizera Muleba.

Afisa Maendeleo ya Jamii Wilayani humo  Bw.Shaban Manyama
amesema mafunzo hayo ni ya  siku mbili ambapo  yamehitimishwa jana ikiwa vikundi  18 ni vya wakina mama, 7 ni vijana na viwiwli vya walemavu.

Bw.Manyama amesema kupitia mafunzo hayo yatasaidia vikundi hivyo
kuongeza uzalishaji katika miradi yao kwenye biashara, utunzaji wa kumbukumbu na ujasiriamali ambapo vikundi hivyo vimetimiza vigezo.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwemo vijana, wanawake
pamoja na walemavu wamesema elimu hiyo itawasaidia kuendeleza
miradi yao na kuachana na tabia ya utegemezi.


Post a Comment

0 Comments