habari Mpya


Utafiti Wabaini Ufaulu wa Chini wa Hisabati, Kiingereza na Kiswahili, wilayani Ngara.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania umebaini kwamba wanafunzi wa darasa la tatu katika shule za msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wanaweza kufaulu masomo ya Kiingereza, heasabu na Kiswahili kwa wastani wa asilimia 31.

Hayo ameyabaini Mkurugenzi wa Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania Bw. Isaiac Bambara wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti uliolenga kujua uwezo wa watoto wa darasa la III katika masomo hayo.

“Tulifanya utafiti huo nchi nzima mwaka mwaka 2015 kwa watoto wenye umri wa miaka 9-13, tukawashirikisha watoto112,455, ambapo Ngara tulikuwa na washiriki 21, 800 kutoka katika kaya 60 na kila kituo kilikuwa na watoto 30 walioshiki.” Alisema Bw. Bambara.
Alisema utafiti huo umebaini kwamba asilimia 43 ya watoto wa darasa la II wanaweza kumudu hesabu za darasa hilo, wanaoweza kusoma hadithi ni asilimia 67 pekee, ambapo asilimia 53 wa darasa la saba ndio wanaweza kufanya vema hesabu za darasa la II.

Bw. Bambara amethibitisha kwamba watoto wa darasa la saba wanaoweza kusoma vitabu vya hadithi za kiingereza vya dararsa la II ni asilimia 42 pekee.

Aidha, utafiit huo ulilenga pia kujua mahudhurio ya Walimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, kadiri ya Bw. Bambara wamebaini kwamba walimu wanahudhuria kazini kwa wastani wa asilimia 84, huku watoto wakihudhuria kwa wastani wa asilimia 52 tu.

Bw.Baramba amesema kwamba lengo kubwa ni kushirikiana kuhakikisha watoto wanafaulu kwa kiwango kinachotakiwa, hivyo utafiti huo uwe chachu ya kuboresha miundombinu na mazingira rafiki ya kufundidhia.
Amebainisha kwamba Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania (MAT) limetumia Zaidi ya shilling milioni 19, ambapo Shirika la Twaweza Uwezo limechangia shilingi 1.3 zilizotumika kuandaa ripoti ya utafiti huo.

Akishukuru Shirika la MAT, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bw. Gideon Mwesiga, amesema kwamba utafiti huo utawahamasisha walimu kufanya kazi kwa kujituma, juhudi na maarifa na hatimaye watoto watafanyavizuri katika masomo yao.

 Amesema shule nyingi za msingi katika Halmashauri yake zinakabiliwa na upungufu wa vitabu vya darasa la IV, na kwamba matumaini yapo kwani serikali imeanza kuvisambaza katika baadhi ya mikoa, kama ule wa Pwani.

Post a Comment

0 Comments