habari Mpya


Unit 221 za Damu Zapatikana kutoka kwa Wananchi wilayani Kibondo mkoani Kigoma.

Damu iliyochangwa na Wananchi wa Kibondo ikiwa tayari kwenda Kufanyiwa taratibu zingine kabla ya kuanza kutumika kwa Wagonjwa wahitaji.


Picha na Team Damu Salama/Radio Kwizera.

Jumla ya Unit 221 za damu zimepatikana kutoka kwa Wananchi wakati wa muendelezo wa zoezi la Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchangia damu kwa hiari May 19, 2018 kwenye Viwanja vya Community Center na Hospitali ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.
 
Mkuu wa wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Bw. Louis Peter Bura na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya wilaya hiyo Bw.Juma Mnwele waliwaongoza wakazi wa mji wa Kibondo na maeneo jirani kuchangia damu katika kampeni inayoendeshwa na Radio Kwizera  FM ya wilayani Ngara mkoani Kagera.

 Wananchi wa Kibondo wakichangia Damu Jana May 19,2018.

Bw Bura amesema katika wilaya hiyo mahitaji ya damu ni makubwa kwa Hospitali ya wilaya, Vituo vya Afya Vitatu na Zahanati 38 ambapo watoto wachanga, wajawazito wanaohitaji kujifungua na wanaopata ajali ndio wahanga na kwamba  damu hiyo itasaidia wagonjwa hao katika hospitali na vituo vya Afya wilayani Kibondo.   


Nae Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Bw.Juma Mnwele ameishukuru Radio Kwizera katika uhamasishaji wananchi kuchangia damu na kwamba wastani wa mahitaji ya damu  ni unit 300 mpaka 350 kwa mwezi kwa hospitali na vituo vya afya wilayani humo. 


Post a Comment

0 Comments